1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Miito yatolewa kuwepo na kipindi cha mpito Sudan

9 Aprili 2019

Mataifa ya Magharibi yameungana na waandamanaji wa Sudan wanaodai mpango wa mpito wa kisiasa huku jeshi likiachana kuwatawanya waandamanaji waliopiga kambi nje ya makao makuu yao.

https://p.dw.com/p/3GWcq
Sudanesen protestieren in Dublin
Picha: picture-alliance/NurPhoto/A. Widak

Maelfu ya waandamanaji wakiimba nyimbo za "uhuru, uhuru" walibakia nje ya makao makuu ya jeshi mjini Khartoum kwa siku ya nne siku ya Jumanne, baada ya vikosi vya usalama kuanchana na juhudi zao kuwatawanya kufuatia uingiliaji wa jeshi kuwalinda waandamanaji hao, kwa mujibu wa watu walioshuhudia.

"Wakati umefika kwa mamlaka za Sudan kujibu matakwa haya ya umma katika njia ya maana na ya kuaminika," balozi za Marekani, Uingereza na Norway zilisema katika taarifa ya pamoja.

"Serikali ya Sudan sasa inapaswa kuitikia na kuwasilisha mpango unaoaminika kwa ajili ya mpito huu wa kisiasa," waliongeza.

Maelfu wamekuwa wakiandamana tangu Jumamosi nje ya makao makuu ya jeshi ambayo pia yanahifadhi makaazi ya rais, katika maandamano makubwa zaidi tangu kuzuka kwa maandamano dhidi ya kupanda kwa bei ya mkate mwezi Desemba.

Maandamano hayo tangu hapo yamesambaa kwenye miji midogo na mikubwa katika taifa hilo la kaskazini-mashariki mwa Afrika, na kutanua madai yao kumtaka Bashir aachie ngazi.

Omar al-Bashir
Maji yamefika shingoni: Rais Hassan Omar al-Bashir.Picha: picture-alliance/AP Photo/H. Ammar

Mapema Jumanne, maafisa wa idara ya taifa ya intelijensia na huduma za usalama na polisi wa kuzuwia ghasia walifyatua risasi katika jaribio lililoshindwa la kukomesha maandamano hayo, alisema moja wa waandaji wa vuguvugu hilola maandamano.

Waziri wa ulinzi Jenerali Awad Ibnouf aliapa kuwa jeshi litazuwia kutokea kwa machafuko.

" Vikosi vya jeshi la Sudan vinafahamu sababu za waandamanaji na halipingi madai hayo na matakwa ya wananchi, lakini halitoruhusu nchi kutumbukia kwenye machafuko," Ibnouf alisema Jumatatu, akinukuliwa na shirilarasmi la habari la Sudan SUNA.

Katika taarifa tofauti, mnadhimu mkuu wa jeshi Kamala Abdelmarouf alisema jeshi lilikuwa linatekeleza wajibu wake wa kuhakikisha usalama wa raia.

Maafisa wanasema watu 38 wameuawa katika maandamano tangu Desemba.

Baada ya kikao kilichoongozwa na Bashir siku ya Jumapili, baraza la usalama la Sudan lilisema madai ya waandamanaji "hayajasikika."

chanzo: afpe.