1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIsrael

Israel: Waliokufa Oktoba 7 walikuwa ni 1,200

11 Novemba 2023

Israel imebadilisha idadi ya vifo vilivyotokea kwenye shambulizi la Oktoba 7, kutoka watu 1,400 hadi 1,200.

https://p.dw.com/p/4YgrG
Israel imeendelea kushambulia Ukanda wa Gaza kufuatia operesheni ya klijeshi baada ya shambulizi la Hamas la Oktoba 7
Israel imeendelea kushambulia Ukanda wa Gaza kufuatia operesheni ya klijeshi baada ya shambulizi la Hamas la Oktoba 7Picha: Leo Correa/AP Photo/picture alliance

Hayo yameelezwa na msemaji wa Wizara ya mambo ya Kigeni ya nchi hiyo Lior Haiat alipozungumza na shirika la habari la AFP.

Amesema idadi hiyo ya vifo 1,200 ndiyo halisi na ile iliyotolewa awali ilijumuisha wanamgambo wa Hamas waliouwawa ambao wamefahamika baada ya zoezi la utambuzi wa miili kukamilika.

Katika hatua nyingine, viongozi wa Afrika wametoa Azimio la pamoja kwenye mkutano wa kilele wa Maendeleo mjini Riyadh linaloelezea wasiwasi kuhusiana na hali ya kiutu huko Gaza na kutoa wito wa kumalizwa operesheni ya kijeshi na raia kulindwa.

Azimio hilo linaungwa mkono na Mwanamfalme wa Saudia, Mohammed bin Salman, aliyezungumza kwa mara ya kwanza tangu mzozo huo ulipoanza, ambaye pia ametaka sheria za kimataifa kulindwa.