1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Miili 28 ya watu waliouwawa yapatikana Burkina Faso

3 Januari 2023

Waendesha mashtaka nchini Burkina Faso wamesema miili ya watu 28 waliouawa kwa risasi imepatikana katika mji wa Kaskazini Magharibi mwa nchi hiyo wa Nouna.

https://p.dw.com/p/4Lfqz
Burkina Faso Gendarmerie nationale
Picha: SIA KAMBOU/AFP via Getty Images

Uchunguzi umeanzishwa kuhusiana na mauaji hayo yaliotokea Desemba 30, wamesema waendesha mashtaka hao katika taarifa bila kutoa ufafanuzi zaidi kuhusu waliofanya uhalifu huo na dhumuni lao.

Taifa hilo la Afrika Magharibi linapambana dhidi ya uasi wa wapiganaji wa jihadi ambao umesambaa kutoka nchi jirani ya Mali katika muongo uliopita.

Maelfu ya watu wameuawa kote katika kanda hiyo, na mamilioni wamelaazimika kuyapa kisogo makazi yao.