1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MichezoNew Zealand

Michuano ya Kombe la Dunia la wanawake yaanza

20 Julai 2023

Michuano ya Kombe la Dunia la Kandanda kwa Wanawake inafungua pazia leo kwa mchezo wa ufunguzi utakaozikutanisha New Zealand na Norway mjini Auckland. New Zealand inaongoza kwa bao 1-0.

https://p.dw.com/p/4U9vc
FIFA Frauen Fußball WM | Neuseeland vs Norwegen | Tor 1:0
Picha: Phil Walter/Getty Images

Hata hivyo, katika dakika ya 87, New Zealand ambao ni wenyeji wa michuano hiyo, kupitia mchezaji wake Ria Percival walikosa mkwaju wa penalti.

Ufunguzi wake nusura uingie kiwingu baada ya watu watatu kuuwawa na mshambuliaji aliyefyatua ovyo risasi mjini Auckland. Mtu huyo alitumia silaha yake kwenye eneo moja la ujenzi karibu na ngome ya mashabiki wanaosubiri kwa shauku kuanza kwa kombe la dunia la wanawake.

Serikali ya New Zealand na Shirikisho la Kandanda Duniani, FIFA wamesema kwa pamoja kuwa mchezo wa ufunguzi utaendelea kama ulivyopangwa. Pande zote mbili pia zimetuma salamu za pole kwa familia za walipoteza wapendwa wao.

FIFA imesema tukio hilo halina uhusiano na tamasha hilo la michezo na waziri mkuu wa nchi hiyo Chris Hipkins hakuna kitisho chochote kwa usalama wa taifa kutokana na kisa hicho.