1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Michezo ya makundi katika Ligi ya mabingwa Ulaya kupangwa

Sekione Kitojo
29 Agosti 2018

Real Madrid mabingwa watetezi, na mahasimu wao Atletico Madrid na Barcelona  ni miongoni mwa timu za juu zitakazokuwa  katika chungu namba 1 kwa ajili ya upangaji wa makundi katika kinyang'anyiro cha Champions League.

https://p.dw.com/p/33wEm
UEFA Champions League Pokal
Picha: picture-alliance/Mandoga Media

Mabingwa  mara  tatu mfululizo  ambao  ndio  mabingwa  watetezi  kwa  sasa katika  Champions League  Real Madrid , ambao  kwa  sasa  wanacheza  bila ya  Cristiano Ronaldo, mabingwa  wa  kombe  la  ligi  ya  Ulaya  Atletico Madrid  na  Barcelona  ni  miongoni  mwa  timu za  juu  katika  upangaji  wa awamu  ya  makundi  katika  Champions League unaofanyika  Alhamis (30.08.2018).

UEFA Super Cup 2018 | Real Madrid v Atletico Madrid | Torjubel (1:1)
Wachezaji wa Real Madrid wakimpongeza Gareth BalePicha: Getty Images/A. Hassenstein

Chungu namba  moja  kinajumuisha  klabu  mpya  ya  Ronaldo Juventus , timu  mbili ambazo zina nia  ya  kulinyakua  kombe  hilo  kutoka  mji  wa Manchester  pamoja  na  Paris  Saint-Germain, Bayern  Munich  na  Lok Moscow.

Kwa  mara  ya  kwanza  ligi  za  juu  za  Uingereza , Italia, Uhispania  na Ujerumani  zitakuwa  na  timu  nne  zilizomaliza  nafasi  za  juu  kutoka  katika msimu  uliomalizika   zikiingia  moja  kwa  moja  katika  awamu  ya  makundi, ambazo zitachezwa  kuanzia  Septemba 18  hadi  Desemba 12.

Kama  ilivyokuwa  huko  nyuma, timu  kutoka  katika  ligi  moja  zitawekwa mbali  katika  upangaji  huu  mjini  Monaco siku ya Alhamis.

UEFA Super Cup 2018 | Real Madrid v Atletico Madrid
Mabingwa wa ligi ya Ulaya Atletico Madrid ya UhispaniaPicha: Reuters/I. Kalnins

Timu  hizo 32 zimegawanywa  katika  vyungu vinne vya  timu  nane, ambapo chungu  namba  moja  kitakuwa  na  mabingwa  watetezi Real Madrid, mabingwa  wa  ligi  ya  Ulaya  Atletico Madrid na  mabingwa  kutoka  katika katika  nchi  sita za  juu  kabisa  katika Ulaya.

Vyungu vingine 4

Timu  nyingine  24  zimewekwa  katika  vyungu namba  mbili  hadi  4 kwa mujibu wa  uwezo  wa  klabu, wakati  Borussia  Dortmund  na  Manchester United  ni  miongoni  mwa  timu  zilizoko  katika  chungu  namba  2, monaco na  Ajax zimo  katika  chungu  namba  3, na  Galatasaray  na  Inter Milan  ya Italia  zimo  katika  chungu  namba  4.

Makamu  bingwa  wa  kombe  la  ligi ya mabingwa  msimu  uliopita  Liverpool itakuwa  katika  chungu  namba  2  ama  3, ikitegemea  na  matokeo  ya michezo  ya  mwisho  ya  mechi  za mchujo jioni  ya  Jumatano.

Liverpool FC vs  Borussia Dortmund
Wachezaji wa Liverpool wakishangiria bao dhidi ya Manchester City katika Champions LeaguePicha: picture-alliance/dpa/P. Powell

Ronaldo  ni  mfungaji  bora  katika  Champions League  katika  misimu mitatu  iliyopita, akiwa  na  mabao 120. Pia  ameshinda  tuzo ya  goli  la msimu  katika  bao  lake  la tikitaka  katika  ushindi  wa  Real wa  mabao 3-0 dhidi  ya  Juventus, ambapo shangwe  zilizotoka upande  wa mashabiki  wa Juventus zimemfanya amue  kujiunga  na  mabingwa  hao  wa  Italia.

Juve  watakuwa  na  matumaini  kwamba  Ronaldo anaweza  kuwasaidia kushinda  taji  hilo  la  juu  katika  soka  la  Ulaya  kwa  mara  ya  kwanza  tangu mwaka  1996, baada  ya  kushindwa  katika  fainali nne tangu  wakati  huo, ikiwa  ni  pamoja  na  mwaka  2015 na  2017.

Kwa upande  wao Real , hivi  sasa  inapaswa  kumtegemea Karim Benzema na  Gareth Bale ambao  hata  hivyo  wamefanikiwa  kupata  mabao  wakati Real  ilipoishinda  Liverpool  3-1 kwa  ubingwa  mara  13  katika  champions League. Pia  wana  kocha  mpya  Julen Lopetegui  baada  ya  kuondoka Zinadine  Zidane.

Champions League Final - Real Madrid v Liverpool - Zinédine Zidane
Kocha wa zamani wa Real Madrid Zinedine ZidanePicha: Imago/Newspix/R. Oleksiewicz

Pep Guardiola  wa  Man City  na  PSG, ambao  sasa  wana  kocha  mpya Thomas Tuchel  raia  wa  Ujerumani , wanataka  kunyakua  kombe  hilo hatimaye  baada  ya  kufanya  vibaya  katika  misimu  iliyopita licha  ya  utajiri wao.

Mwandishi: Sekione  Kitojo / dpae

Mhariri: Iddi Ssessanga