Miaka 43 ya Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar
26 Aprili 2007Matangazo
Hata hivyo miaka ya karibuni imeshuhudia kuzidi kwa manung'uniko kutoka pande zote mbili juu ya kasoro mbali mbali ikiwa ni pamoja na muundo wa muungano wenyewe. Miongoni mwa hoja ni ukosefu wa ridhaa ya wananchi wa pande zote mbili na kutofahamika kwa uwazi kama kulikuweko na waraka uliounda muungano huo au la.
Abubakar Liongo amezungumza na Katibu wa kwanza wa Baraza la mapinduzi Zanzibar Balozi Salim Rashid na kwanza kuhusu masuala hayo mawili na hali ya muungano wenyewe alikuwa na haya ya kusema.