1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Miaka 10 ya mpango wa Umoja wa mataifa kupambana na umasikini

15 Februari 2006

Wataalamu wasema lengo halijafikiwa.

https://p.dw.com/p/CHnp

Kubwa zaidi ambalo Human rights watch limeitaka Libya kulitekeleza ili kuharakisha mageuzi katika suala la haki za binaadamu ni kuyageuza maneno kuwa vitendo, ili iwajibike n na kuheshjimu sheria aya kimataifa juu ya haki za binadamu.

Ikikaribia miaka 10 tangu Umoja wa mataifa ulipotangaza ”muongo mmoja wa kupambana na umasikini”, bado zaidi ya watu bilioni moja wanaishi katika hali ya ukosefu wa maji safi ya kunywa, huduma ya afya, uhaba wa makaazi na mambo mengine muhimu kwa maisha ya kila siku. Hayo ni kwa mujibu wa mtazamo wa wataalamu na wachunguzi wa kujitegemea wa kimataifa.

“Umasikini ni sawa na ugonjwa wa kuambukiza ambao unazagaa kote dunian” Hayo yalitamkwa na Jesus Gamboa katika mkutano wa umoja wa mataifa mjini New York, ulioitishwa kutathimini maendeleo yaliopatikana katika kipindi cha muongo mmoja katika juhudi za kupunguza umasikini.

Akiiwakilisha jumuiya moja ya kiraia kutoka Philippines, Gamboa mwenye umri wa miaka 17, alisema si yeye wala yeyote katika familia yake na marafiki mwenye taarifa kuhusu kampeni ya kupambana na umasikini. Kwa maneno mengine hawaoni kama kuna maendeleo yoyote.

Mkutano huo wa kutathimini maendeleo yaliopatikana katika jitihada za kupunguza umasikini tokea 1997-2006,ambao ni wa kwanza kuitishwa na tume ya maendeleo ya jamii unaendelea hadi ksesho Ijumaa.

Kampeni ya umoja wa mataifa dhidi ya umasikini ilianzishwa kutokana na maamuzi yaliopitishwa katika mkutano wa kilele wa maendeleo ya jamii duniani uliofanyika Copenhagen-Denmark 1995, ambako viongozi wa dunia walikubaliana kuandaa mipango ya ushirikiano pamoja na jumuiya ya kimataifa kupambana na umasikini, ukosefu wa ajira na tabia ya watu kutengwa katika jamii.

Lakini wakati muongo huo ukikaribia kumalizika, wahusika ndani ya umoja wa mataifa pamoja na wataalamu, wawakilishi wa jumuiya za kiraia na wa mashirika yasio ya kiserikali wanayaona matokeo kuwa yasiotosha.

Naibu katibu mkuu anayehusika na masuala ya uchumi na jamii Jose Antonio Ocampo alisema wakati wa ufunguzi wa kikao hicho wiki iliopita, kwamba licha ya hatua ya maendeleo , tume imeshindwa kufikia malengo yaliowekwa kufuta umasikini. Pamoja na kutaja juu ya kupunguzwa kwa sehemu kubwa umasikini katika maeneo ya mashariki na kusini mwa Asia na pia Pacific, Bw Ocampo alisema maeneo yote mengine yamepata pigo tangu 1990. Alisema masikini mkubwa bado ungaliko katika nchi nyingi na hasa zile za Afrika, kusini mwa jangwa la Sahara.

Ripoti ya Shirika la mpango wa maendeleo la umoja wa mataifa UNDP kuhusu maendeleo ya binaadamu 2005 inasema kwamba ,baada ya miaka kumi tangu kutangazwa vita dhidi ya umasikini, bado zaidi ya 40 asili mia ya wakaazi duniani wanakabiliana kila siku na hali halisi ya moja kwa moja au kitisho cha umasikini. Azma ya kupambana na umasikini, ilisisitizwa kwa sauti kubwa na nchini wanachama wa umoja wa mataifa, hasa kupitia utekelezaji wa malengo ya maendeleo ya milenia yaliofafanuliwa katika mkutano wa kilele wa milenia wa umoja wa mataifa mwaka 2000.

Malengo manane ya milenia ni pamoja na kupunguza umasikini na njaa kwa 50 asili mia, elimu ya mingi kwa wote, kupunguza vifo vya watoto kwa theluthi mbili, kupunguza vifo wakati wa uzazi kwa robo tatu, usawa wa jinsia, ulinzi endelevu wa mazingira, na kupambana na ukimwi, malaria na magonjwa mengine pamoja na ushirikiano wa kimataifa kwa ajili ya maendeleo-kati ya nchi tajiri na masikini-huku yote yakilengwa kufikiwa ifikapo 2015.

Wachambuzi wanasema licha ya uwezo wa dunia na kujitolea kwake katika kupunguza umasikini kwa nusu ile idadi ya watu wanaoishi katika umasikini uliokithiri ifikapo 2015, chini ya mpango wa maendeleo wa milenia, haielekei kama malengo hayo yatafikiwa mna nchi nyingi na maeneo mengi duniani.

Hoja zinazotajwa ni kuwa nchi tajiri hazifanyi wajibu wao kwa sababu gharama ya kufikia malengo hayo inaonekana kuwa ni kubwa mno bila ya kuzingatia kwamba gharama ya kutofuta umasikini ni hata kubwa zaidi. Wanahoji kwamba kwa sasa yamekua magumu kwa nchi zinazoendelea kwa sababu ya kulazimishwa kufuata mfumo wa kiuchumi ambao hauendani na mahitaji yao .