1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiUganda

Mgonjwa wa mwisho wa Ebola aondoka hospitali Uganda

2 Desemba 2022

Mgonjwa wa mwisho aliyetambulika kuugua ugonjwa wa Ebola ameruhusiwa kuondoka hospitalini.

https://p.dw.com/p/4KP2n
Uganda Battles Seventh Ebola Outbreak Since 2000
Picha: Luke Dray/Getty Images

Mgonjwa wa mwisho aliyetambulika kuugua ugonjwa wa Ebola ameruhusiwa kuondoka hospitalini.

Afisa mmoja mkuu wa afya Diana Atwine, amesema hayo leo na kuongeza matumaini kwamba mlipuko wa ugonjwa huo ambao umeua

takriban watu 56 huenda ikawa unakaribia kumalizika.

Atwine amesema maafisa wa afya wataendelea kuwafuatilia watu waliotangamana na walioambukizwa hadi watakapobainika kutokuwa na maambukizi baada ya siku 21. Hata hivyo, hakusema ni lini kisa cha mwisho kilithibitishwa .

Maafisa kwanza walithibitisha mripuko wa ugonjwa huo mnamo mwezi Septemba na kusema virusi vya ugonjwa huo vilikuwa vya aina ya Sudan inayosababisha vifo vya asilimia 40 hadi 60 ya wale walioathirika na ambayo haina chanjo iliyoidhinishwa.