1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiMamlaka ya Palestina

Mfungwa maarufu wa Kipalestina afariki baada ya kugoma kula

2 Mei 2023

Idara ya magereza nchini Israel imesema mfungwa maarufu wa Kipalestina, Khader Adnan, amefariki leo akiwa chini ya ulinzi wa Israel baada ya kuendeleza mgomo wa kususia kula kwa kiasi miezi mitatu.

https://p.dw.com/p/4QnOD
Trauer um Khader Adnan, einem palästinensischen Gefangenen, der im israelischen Gefängnis starb
Picha: Majdi Mohammed/AP

Tukio hilo limekuja katika wakati ambapo tayari mvutano umeongezeka kati ya Israel na Wapalestina.

Kifo cha Adnan kimeongeza uwezekano wa kuzuka upya machafuko kati ya Israel na makundi ya wanamgambo ya Kipalestina  wakati vurugu zikiongezeka katika Ukingo wa Magharibi. 

Muda mfupi baada ya kifo cha mfungwa huyo kutangazwa, wanamgambo Wakipalestina katika ukanda wa Gaza  walifyetuwa maroketi kuelekea Kusini mwa Israel.

Aidha wapalestina wameitisha mgomo mkubwa katika Ukingo wa Magharibi na Ukanda wa Gaza na maandamano yanatarajiwa baadae leo.

Khader Adnan aliyekuwa kiongozi wa kundi la wanamgambo la Jihad ndani ya Palestina ni mfungwa wa kwanza kufa tangu wafungwa wakipalestina kuanzisha mgomo wa kula katika kipindi cha kiasi muongo mmoja.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW