1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mfumuko wa bei waongezeka zaidi nchini Sudan

Yusra Buwayhid
19 Julai 2021

Mfumuko wa bei umeongezeka nchini Sudan na kupindukia asilimia 400, kulingana na vyombo vya habari nchini humo, huku kukiwa na malalamiko mengi dhidi ya bidhaa kupanda bei kufuatia mageuzi ya kiuchumi

https://p.dw.com/p/3wgY6
Sudanesisches Pfund, 1-Pfund-Banknote
Picha: imageBROKER/picture alliance

Mfumuko wa bei umeongezeka nchini Sudan na kupindukia asilimia 400, kulingana na vyombo vya habari nchini humo, huku kukiwa na malalamiko mengi dhidi ya bidhaa kupanda bei kufuatia mageuzi ya kiuchumi yaliyofanywa na serikali ikiungwa mkono na Shirika la Fedha Duniani (IMF).

Sudan imekuwa ikipitia kipindi kigumu cha mpito tangu Agosti 2019 baada ya kuondolewa madarakani Rais Omar al-Bashir kufuatia maandamano ya umma yaliyochochewa na ugumu wa kiuchumi.

Serikali ya mpito iliyoingia madarakani Agosti 2019, imeahidi kuimarisha uchumi ulioharibiwa na vikwazo vya Marekani na usimamizi mbaya wa Bashir.

Hatua za kiuchumi zilizochukuliwa na serikali hiyo mpya zinaangaliwa na Wasudan wengi kuwa ni kali. Lakini ni sehemu ya maguezi yaliyopendekezwa na IMF kuliwezesha taifa hilo kusamehewa madeni yake.