1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mfumo wa TEHAMA watetereka na kuzusha kizaazaa duniani

Sylvia Mwehozi
19 Julai 2024

Biashara na taasisi nyingi kote ulimwenguni zimeshuhudia kukatika kwa mawasiliano baada ya kutokea hitilafu kubwa katika mfumo wa TEHAMA.

https://p.dw.com/p/4iVOi
Mfano wa mfumo wa mawasiliano ya TEHAMA
Hitilafu kwenye mfumo wa TEHAMA umeleta kizaazaa kila kona duniani. Picha: Sebastian Gollnow/dpa/picture alliance

Mabenki, maduka makubwa na taasisi nyingine kote duniani, zimeripoti kukatika kwa huduma zinazohusisha intaneti, huku baadhi ya mashirika ya ndege yakitoa tahadhari ya kucheleweshwa au kusitishwa safari za ndege.

Tatizo hilo limeathiri safari za ndege nchini Marekani, limetatiza matangazo ya televisheni nchini Uingereza na limeathiri mawasiliano ya simu nchini Australia. Uwanja wa ndege wa Brandenburg nchini Ujerumani, pia umetangaza kusitisha baadhi ya safari za ndege.

Kampuni kubwa ya teknolojia ya Microsoft imesema usiku wa kuamkia leo kuwa inachunguza tatizo hilo, ambalo limeathiri huduma na programu zake na kuongeza kwamba watumiaji wake watashindwa kuzifikia huduma nyingi zinazotegemewa na mamilioni ya watu duniani kote.