1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaMorocco

Mfalme wa Morocco awatembelea manusura wa tetemeko la ardhi

13 Septemba 2023

Mfalme wa Morocco Mohammed VI amedhirisha mshikamano kwa taifa lake lililo kwenye majonzi, kwa kuchangia damu na kuwatembelea hapo jana baadhi ya majeruhi katika hospitali moja mjini Marrakesh.

https://p.dw.com/p/4WGUt
Marokko | König Mohammed IV
Picha: Alexander Shcherbak/TASS/dpa/picture alliance

Uchangiaji wa damu umekuwa ishara ya kitaifa ya mshikamano, na raia wa Morocco wamekuwa wakipanga foleni huko Marrakesh na katika miji mingine ili kuwachangia damu waliojeruhiwa.

Baadhi ya raia wa  Morocco wanailamu serikali kwa kuchelewesha shughuli za uokoaji. Tetemeko la ardhi nchini Morocco limesababisha hadi sasa vifo vya watu zaidi ya 2,900 huku maelfu ya wengine wakijeruhiwa.