1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mfalme wa Jordan ahimiza usitishaji mapigano Gaza

7 Januari 2024

Mfalme Abdullah wa pili wa Jordan amemtaka Anthony Blinken ashinikize usitishwaji wa mapigano katika Ukanda wa Gaza.

https://p.dw.com/p/4ax70
Jordanien König Abdullah II and Kronprinz Hussein  U.S. Aussenminister Antony Blinken in Amman
Mfalme Abdullah wa pili wa Jordan, wa pili kutoka kulia, na Anthony Blinken, wa pili kutoka kushoto.Picha: Royal Hashemite Court/Handout via Reuters

Mfalme Abdullah wa Pili wa Jordan amemhimiza Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Athony Blinken ashinikize usitishwaji mapigano katika Ukanda wa Gaza na kufikisha mwisho mzozo wa kibinadamu uliosababishwa na miezi mitatu ya vita. Mfamle Abdulla wa Pili ametoa kauli hizo kwa Blinken ambaye anafanya ziara ya nne Mashariki ya Kati inayolenga kuhakikisha vita kati ya Israel na Hamas havisambai.

Mfalme huyo pia amemuonya Blinken juu ya athari za mashambulizi yanayoendelea Gaza, akisisitiza umuhimu wa kuufikisha mwisho mgogoro wa kibinaadamu Gaza. Amesisitiza jukumu muhimu la Marekani katika kushinikiza makubaliano ya haraka ya usitishwaji mapigano Gaza, kuwalinda raia na hakikisho la upelekaji misaada ya matibabu na kibinaadamu.