1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mfalme Charles lll amekula kiapo na kuvikwa taji

6 Mei 2023

Mfalme Charles lll amekula kiapo na amevikwa taji kwenye sherehe iliyohudhuriwa na maalfu ya wageni na watu mashuhuri kwenye kanisa la Anglikana la Westminster, Abbey jijini London.

https://p.dw.com/p/4Qzc0
London Krönung König Charles
Picha: Julian Simmonds/REUTERS

Mfalme Charles wa tatu amekula kiapo na amevikwa taji kwenye sherehe iliyohudhuriwa na maalfu ya wageni na watu mashuhuri kwenye kanisa la Anglikana la Westminster, Abbey jijini London. Mamilioni ya watu duniani kote pia walifuatilia hafla hiyo. Charles alianza kukalia kiti cha ufalme tarehe 8 mwezi Septemba mwaka uliopita baada ya kifo cha mama yake Malkia Elizabeth wa pili. Mke wa Charles Camilla pia amevishwa taji la umalkia kwenye sherehe ya leo. Viongozi wa dunia, waliomo madarakani na wastaafu walikuwapo kanisani kushuhudia kuvikwa taji kwa Mfalme Charles wa tatu. Miongoni mwao rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, waziri mkuu wa Australia Anthony Albanese na waziri mkuu wa Canada Justin Trudeau. Mke wa rais wa Marekani Jill Biden pia alihudhuria sherehe hiyo. Ujerumani iliwakilishwa na rais wake Frank-Walter Steinmeier.