1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mfalme Charles kuanza ziara Ujerumani

28 Machi 2023

Mfalme Charles III wa Uingereza ataanza ziara yake ya kwanza rasmi nchini Ujerumani siku ya Jumatano baada ya kuakhirisha kwenda nchini Ufaransa kutokana na kuenea kwa maandamano ya kisiasa nchini humo.

https://p.dw.com/p/4PMx0
BdTD I Frankreich I König Charles III aus Wachs im Museum Grevin in Paris
Picha: Thomas Samson/AFP/Getty Images

Katika ziara hiyo ya siku tatu, Mfalme huyo wa Uingereza ataanzia kwanza Berlin atakakofanya shughuli kadhaa kabla ya kuelekea mjini Hamburg.

Rais wa Ujerumani Frank Walter Steinmeier amesema ziara hiyo inaonesha urafiki wa karibu kati ya nchi hizo mbili na raia wao. 

Mfalme Charles na mkewe Camilla watapokelewa na Rais Steinmeier pamoja na mkewe Elke Buedenbender kwa heshima za kijeshi katika eneo la kihistoria la lango la Brandenburg mjini Berlin.

Ziara hiyo inaangaliwa kama juhudi za Uingereza kujaribu  kujenga mahusiano na majirani zake baada ya nchi hiyo kuondoka kwenye Umoja wa Ulaya.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW