1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mfalme Charles III wa Uingereza atoa hotuba ya kwanza

10 Septemba 2022

Mfalme Charles III wa Uingereza amehutubia taifa lake kwa mara ya kwanza tangu kutokea kifo cha mama yake Malkia Elizabeth II.

https://p.dw.com/p/4GexE
Großbritannien König Charles III
Picha: Yui Mok/Pool Photo via AP/picture alliance

Katika hotuba yake hiyo aliyoitoa katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Paulo, tangu awe mfalme alimtaja Malkia Elizabeth kuwa ni mtu wa mfano kwake na familia yao kwa ujumla.

Kutokana na yale yote aliyoyatenda mama yake, amesema yanaonesha kuwa wana deni lake la dhati kwa kutimiza  upendo na mwongozo.

Mfalme Charles III ameonesha nia ya dhati kwa kuanza majukumui yake kama mfalme kwa kuendeleza huduma ya maisha yote ya mfano wa Malkia Elizabeth II kwa zingatio la hali ya sasa, chini ya enzi mpya.

Ahadi ya kuwahudumia Waingereza.

UK Queen Elizabeth II gestorben Buckingham Palace | Charles kommt an
Mfalme Charles III akisalimiana na watu wa LondonPicha: Ben Stansall/AFP

Katika hotuba dakika tisa na nusu ambayo ilirekodiwa awali, akiwa na picha ya malikia mbele yake alitoa ahadi ya kuwahudumia waingereza kwa maisha yake yote, kuanzia sasa.

Amesema kama ilivyokuwa kwa malkia mwenyewe alivyofanya majukumu yake kwa kwa ibada isiyoyumba, na yeye pia, anajitolea kwa dhati, katika muda wote uliosalia ambao Mungu atamjalia kwa kuzingatia kanuni za kikatiba katika moyo kwa moyo wa taifa lao.

Hotuba ya mfalme ilitangazwa kwenye televisheni na mitandaoni kutoka katika Kanisa kubwa la  Mtakatifu Paulo ambapo watu wapatao 2,000 walihudhuria ibada hiyo ya ukumbusho kwa malkia.

Miuongoni mwa watu wengine ibada hiyo ilihudhuriwa na Waziri Mkuu Mpya wa Uingereza Liz Truss na maafisa katika serikali yake, pamoja na mamia ya umma ambao ulijipanga kwa ajili ya kukata tiketi ya kuingilio.

Mkutano wa Mfalme Charles III na Waziri Mkuu Liz Truss

Großbritannien König Charles III mit Premierministerin Liz Truss
Mfalme Charles III na Waziri Mkuu Liz TrussPicha: Yui Mok/Pool photo/AP/picture alliance

Katika hatua nyingine ya awali mfalme huyo alikutana na Wazri Mkuu Liz Truss na kumweleza alikuwa akiiogpa sana siku ambayo amempoteza mama yake, kwa hivyo lazima sasa lazima ahakikishe anajairibu na kufanya kila jambo linakwenda sawasawa. Mkutano wake ulifanyika mjini London. Malkia Elizabeth alimteua Truss siku mbili tu kabla ya kifo chake.

Katika kipindi hiki ambacho Uingereza inaanza kipindi cha maombolezo cha siku 10, watu kutoka katika pande tofauti za ulimwengu wanakusanyika katika balozi za  Uingereza kwa ajili ya kutoa heshima kwa malkia, ambaye

alifariki Alhamisi katika Kasri la Balmoral huko Scotland baada ya miaka 70 ya uongozi wake.

Mjini London na katika maeneo ya kijeshi kote Uingereza, mizinga ilifyatuliwa mara 96 kwa kuonesha heshima kubwa kwa kipindi cha dakika 16 kuashiria kila mwaka wa maisha ya malkia.

Soma zaidi:Truss amwelezea Malkia Elizabeth kuwa mwanadiplomasia mahiri

Charles, ambaye alikua mfalme mara tu baada ya mama yake kufariki, anatarajiwa kuzuru kote nchini Uingereza katika siku zijazo.