1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUingereza

Mfalme Charles III wa Uingereza aanza ziara Ujerumani

Daniel Gakuba
29 Machi 2023

Mfalme Charles III wa Uingereza pamoja na mke wake Camilla wameanza ziara nchini Ujerumani, ya kwanza nje ya Uingereza tangu aliporithi kiti cha ufalme.

https://p.dw.com/p/4PS3E
Deutschland | King Charles III besucht Berlin
Picha: Andreas Rentz/Getty Images

Wamepokelewa na rais wa shirikisho la Ujerumani Frank-Walter Steinmeier na mke wake Elke Büdenbender katika sherehe ya kijeshi kwenye lango maarufu la Brandenburg katikati mwa mji mkuu wa Ujerumani, Berlin. Hii ni mara ya kwanza kwa mgeni yeyote wa Ujerumani kupokelewa katika eneo hilo la kihistoria.

Baadaye, Rais Steinmeier na mke wake Elke Büdenbender watawaandalia karamu ya kifalme wageni wao katika kasri la Bellevue. Ratiba ya kesho katika ziara hiyo ya Mfalme Charles III inaonesha kuwa atapokelewa na Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz na pia Kaimu Meya wa Berlin, Franziska Giffey. Charles III atakuwa mfalme wa kwanza kutoa hotuba katika bunge la Ujerumani.