1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mfalme Charles III aahidi kufuata nyayo za mamake

Saleh Mwanamilongo
12 Septemba 2022

Mfalme Charles wa tatu ameliambia bunge la Uingereza leo kwamba yuko tayari kufuata mifano iliyowekwa na mama yake Malkia Elizabeth wa Pili aliyeaga dunia siku ya alhamisi.

https://p.dw.com/p/4Gjsp
England London | Westminster Hall | King Charles III.
Picha: Henry Nicholls/WPA/Getty Images

Mfalme Charles wa tatu amelihutubia bunge hilo alilolitaja kama mhimili unaoimarisha demokrasia nchini humo. Katika hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa Westminster mjini London, Mfalme huyo mpya wa Uingereza alichukua nafasi hiyo bungeni kutoa heshima zake za mwisho kwa mamake na kuweka ahadi ya kudumisha kanuni za serikali inayoongozwa kikatiba.

Kufariki siku ya alhamis kwa Malkia Elizabeth wa pili aliyeiongoza Uingereza kwa miaka 70, kumefungua muda wa maombolezo ya kitaifa ambapo maelfu ya wakaazi wa Uingereza wanatarajiwa kutoa heshima zao za mwisho kuanzia hapo Kesho Jumanne. Malkia anatarajiwa kuzikwa tarehe 19 Septemba.