1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mfalme Charles azuru Ujerumani

Hawa Bihoga
29 Machi 2023

Mfalme Charles wa III wa Uingereza anakwenda nchini Ujerumani kwa ziara yake ya kwanza rasmi ya nje tangu alipokuwa mfalme wa taifa hilo.

https://p.dw.com/p/4PQC3
UK, Fife | König Charles III und Camilla
Picha: Andrew Milligan/PA/AP/picture alliance

Mfalme Charles anafanya ziara hiyo baada ya kuahirisha ziara yake nchini Ufaransa kutokana na maandamano ya kupinga mabadiliko ya pensheni nchini humo. Katika ziara hiyo ya siku tatu, Mfalme huyo wa Uingereza ataanzia mjini Berlin atakakofanya shughuli kadhaa kabla ya kuelekea mjini Hamburg. Rais wa shirikisho la Ujerumani Frank Walter Steinmeier amesema ziara hiyo inaonesha urafiki wa karibu kati ya nchi hizo mbili. Mfalme Charles na mkewe Camilla watapokelewa na rais Steinmeier pamoja na mkewe Elke Bueden-bender katika gwaride la heshima la kijeshi. Akiwa katika ziara hiyo miongoni mwa mambo anayotarajiwa kugusia ni pamoja na mzozo unaoendelea wa Ukraine.