1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaJordan

Mfalme Abdullah akutana na Netanyahu Jordan

25 Januari 2023

Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, amefanya ziara ambayo haikutangazwa nchini Jordan kwa mazungumzo na Mfalme Abdullah wa II.

https://p.dw.com/p/4MfgE
Deutschland Berlin | König Abdullah II von Jordanien
Picha: Hannibal Hanschke/AFP/Getty Images

Ufalme wa Jordan umesema Mfalme Abdulla alimwambia Netanyahu kwamba Israel inapaswa kuheshimu hadhi ya kisheria na kihistoria ya Msikiti Mtukufu wa Al-Aqsa.

Mfalme huyo wa Jordan amemwambia Netanyahu kwamba kukomeshwa kwa machafuko ni jambo la msingi kuweza kuyakwamua mazungumzo ya amani kati ya Palestina na Israel.

Kulingana na ofisi ya Waziri mkuu wa Israel, viongozi hao wawili walijadiliana pia masuala ya kikanda, hasa ushirikiano wa kimkakati, kiusalama na kiuchumi kati ya Israel na Jordan.

Kurejea madarakani kwa Netanyahu kumezidisha wasiwasi wa Jordan kwamba siasa kali za mrengo wa kulia, ambazo zinajumuisha kuharakisha ujenzi wa makaazi ya walowezi wa Kiyahudi kwenye mamlaka za Palestina, zitachochea wimbi jipya la machafuko.