1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mettlach, Ujerumani. Syria yatakiwa kutoingilia mambo ya ndani ya Lebanon.

5 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCmE

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel na rais wa Ufaransa Jacques Chirac wameitaka Syria kutoingilia mambo ya ndani ya Lebanon.

Katika taarifa ya pamoja iliyotolewa baada ya mkutano wao mjini Mettlach, nchini Ujerumani, viongozi hao wawili wamesema kuwa Syria inapaswa kuchangia kwa njia bora katika juhudi zenye lengo la kuleta amani na uthabiti kwa jirani yake

Merkel na Chirac pia wameeleza kumuunga kwao mkono kwa dhati waziri mkuu wa Lebanon Fouad Siniora. Jana Jumatatu , jeshi la Lebanon liliweka wanajeshi zaidi mjini Beirut baada ya kuuwawa kwa mtu mmoja aliyeshiriki katika maandamano yanayounga mkono Syria na kuzusha hali ya wasi wasi kuwa maandamano hayo dhidi ya serikali yanaweza kuleta ghasia za kimadhehebu.