1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Merz akemea kauli za Makamu wa rais wa Marekani kuhusu Ulaya

15 Februari 2025

Kiongozi wa chama cha upinzani na mgombea wa ukansela nchini Ujerumani Friedrich Merz ameungana leo na vyama vyingine vya ndani ya Ujerumani katika kulaani matamshi ya Vance kuhusu siasa za mrengo mkali wa kulia.

https://p.dw.com/p/4qWM8
 Friedrich Merz
Kiongozi wa chama cha upinzani na mgombea wa ukansela nchini Ujerumani Friedrich MerzPicha: Ronka Oberhammer/DW

Kiongozi wa chama cha upinzani na mgombea wa ukansela nchini Ujerumani Friedrich Merz ameungana leo na vyama vyingine vya ndani ya Ujerumani katika kulaani matamshi kuhusu siasa za mrengo mkali wa kulia yaliyotolewa jana na Makamu wa Rais wa Marekani JD Vance katika mkutano wa kimataifa wa usalama mjini Munich.

Merz amesema Ujerumani ni mlinzi wa uhuru wa kujieleza lakini habari potofu na za chuki hazina nafasi. Mapema leo mpinzani wake ambaye ni Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz aliweka wazi msimamo wake wa kutounga mkono kauli za Makamu wa rais wa Marekani JD Vance aliyekosoa msimamo wa mataifa ya ulaya juu ya demokrasia.

Soma zaidi. Kansela wa Ujerumani asema nchi haitokubali watu wanaoingilia kati demokrasia ya Ujerumani

Ujerumani yenyewe inatazamiwa kufanya uchaguzi wake mkuu mnamo Februari 23 mwaka huu. Kauli za JD Vance kwenye mkutano wa kimataifa wa usalama mjini Munich sio tu kwamba zimewaghadhabisha viongozi wa Ujerumani lakini pia viongozi wa mataifa mengi barani Ulaya.