1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Merkel kuanza kampeni za uchaguzi akiwa dhaifu

3 Aprili 2017

Chama cha Christian Democtratic Union CDU cha kansela wa Ujerumani Angela Merkel kinaelemea zaidi mrengo wa kulia kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2017. Chama hicho kinaazimia kuweka sheria ngumu dhidi ya wahamiaji.

https://p.dw.com/p/2TwgK
Essen CDU-Bundesparteitag Rede Merkel
Picha: picture-alliance/dpa/K. Nietfeld

Mkutano huo  uliofanyika mjini Essen ulitarajiwa kuleta nguvu mpya kwenye chama hicho lakini kuingia kwake katika msimamo mkali au kama wanavyosema wengine  mchezo mchafu kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2017 ilikuwa ni sawa na chama hicho cha CDU kujiweka katika hali ya kusikitisha.  "Muelekeo katika wakati mgumu" ndilo pendekezo llilopitishwa kwa kauli moja na wanachama kuwa ndio hoja kuu itakayo malizia mkutano wa chama hicho iliyopongezwa kwa makofi yaliyodumu kwa sekunde tatu au nne hivi lakini upeo wa furaha ya kisiasa uko tofauti.

Matokeo ya mwisho ambayo yalimwezesha kansela Angela Merkel kuendelea na uenyekiti wa chama cha CDU, ushindi uliotokana hasa na hotuba yake katika mkutano wa chama chake ni kama ilivyokuwa awali. Ushindi wake kwa asilimia 89.5 umefanishwa na "ukweli uliopo" kwamba wengi wa wanachama waliohudhuria  walikuwa ni watu wenye msimamo thabiti juu ya ushindi wa Merkel vile vile makamu wenyeviti walipewa kibarua kigumu ili wasipate fursa ya kumshinda kansela Angela Merkel.

CDU Parteitag in Essen
Wanachama wa CDU katika mkutano wa mjini EssenPicha: Getty Images/S. Gallup

Chama cha CDU  kwa mara ya kwanza kimerejea nyuma katika maudhui yake. Kansela Merkel mwenyewe ametamka kuwa anataka vazi la Burka lipigwe marufuku nchini Ujerumani kauli ambayo iligonga vichwa vya habari ulimwenguni sawa na hapa Ujerumani. Ni mwishoni tu wa mwezi wa Septemba pale Kansela Merkel aliposema kuwa ni kutokana na uhuru wa kuabudu ulipo ndio sababu kubwa iliyokuwa inamfanya apinge hoja ya kupiga marufuku vazi la Burka nchini Ujerumani na badala yake akapendekeza  muongozo maalum kutegemea na mtu hadi mtu.

Jambo jingine ni kuhusu uria pacha. Hatua ya kuanzishwa kwa sheria kali za uhamiaji ikiwemo ya uraia pacha itawaathiri zaidi wahamiaji wa Kituruki ambao wengi wao walikuja hapa Ujerumani tangu miaka ya 60 au 70, walikuja kufanya kazi na baadae waliendelea kuishi humu nchini na hata kupata familia. Kabla ya mwaka 2014 watoto wa wahamiaji walilazimika kisheria wabaki na uraia mmoja pindi tu watakapofikisha miaka 23.

Mwenyekiti wa chama cha Social Demoktratic SPD Sigmar Gabriel pamoja na waziri wa sheria Heiko Maas wamesema hatua hiyo ya kansela Merkel na chama chake inakikua makubaliano yaliyokuwepo awali ambapo watoto wa wahamiaji waliruhusiwa kubakia na uraia pacha, inarudisha nyuma maswala ya kutangamana kwa watu.

Mkuu wa jamii ya Waturuki nchini Ujerumani Goekay Sofuoglu pia amelaani hatua hiyo ya chama cha CDU, akisema kuwa chama hicho kimepoteza maadili yake.

Mwandishi Zainab Aziz/dpae, dw

Mhariri: Gakuba Daniel