1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Merkel hajapata alichotarajia Washington

Sekione Kitojo
28 Aprili 2018

Kansela  Angela Merkel aliwasili kwa mazungumzo na Rais wa  Marekani Donald Trump, yakiwa ni ya pili tangu Trump kuangia madarakani Januari 2017. 

https://p.dw.com/p/2wpgB
USA Washington | Präsident Donald Trump & Angela Merkel, Bundeskanzlerin
Picha: picture-alliance/newscom

Kansela  wa  Ujerumani Angela  Merkel na  rais  wa  Marekani Donald Trump wameeleza tofauti zao kuhusiana  na  biashara na Jumuiya  ya  NATO  katika  mkutano  wao uliofanyika  katika Ikulu  ya White  House  ambako  walijaribu  kuonesha  hali  ya  uchangamfu licha  ya  hali  ya  wasi  swsi  baina  ya  washirika  hao  wawili.

USA Washington | Präsident Donald Trump & Angela Merkel, Bundeskanzlerin
Angela Merkel akiingia Ikulu ya white House pamoja na rais Donald Trump wa MarekaniPicha: Reuters/B. Snyder

Wakati  Trump anakaribia  kuweka ushuru  katika  biadhaa  za chuma na  bati  hivi  karibuni  ambavyo  vitaathiri mauzo  ya  nje  ya mataifa  ya  Ulaya, Merkel  amesema  uamuzi sasa  uko  mikononi mwa  Trump juu  ya  iwapo kutoa  msamaha kwa  mataifa  ya  Umoja wa  Ulaya.

"Tulibadilishana  mawazo. umuazi sasa  una  rais," Merkel aliwaambia  waandishi  habari  baada  ya  Trump  kulalamika  juu  ya kutokuwa  na  uwasa  katika  biashara  kati  ya  Marekani  na  Ulaya, hususan  katika  upande  wa  magari.

Ziara  ya  haraka  ya  Merkel  inakuja  wiki  hiyo  hiyo wakati  wa ziar  ya  siku  tatu  iliyofanywa  na  rais  wa  Ufaransa Emmanuel Macron, ambaye , kama  Merkel, alizungumza  na  trump  kuhusu biashara  na  kumtaka  kuibakisha  Marekani  katika  makubaliano yaliyofikiwa  na  matiafa  kadhaa  ya  kinyuklia  na  Iran.

Hakuna  kiongozi  kati  ya  hao  wawili  aliyeonekana  kupata mafanikio, kumshawishi Trump  katika  masuala  hayo  mawili.

USA Washington | Präsident Donald Trump & Angela Merkel, Bundeskanzlerin
Angela Merkel (kushoto) katika mazungumzo na rais Donald Trump (kulia)Picha: Reuters/K. Lamarque

Uhusiano wa kibiashara wenye uwiano

Merkel  amesema anaweza  kuona  majadiliano  ya  makubaliano  ya kibiashara  kati  ya  Umoja  wa  Ulaya  na  Marekani, akisema shirika  la  biashara la  dunia , WTO halijaweza  kufanikisha makubaliano  ya  kimataifa.

Trump  alisema  anataka  uhusiano  wa  kibiashara  unaowiana  zaidi na  Ujerumani  na  mataifa  mengine  ya  Umoja  wa  Ulaya  na anataka  Ujerumani  na  mataifa  mengine  washirika  wa  NATO walipie fedha  zaidi  kwa  ajili  ya  ulinzi  wao, suala  ambalo hulizusha  mara  kwa  mara.

Tunahitaji uhusiano wa pande  zote mbili,wenye kutendeana vizuri ambao hatuna. Tunafanyakazi kufanikisha  hali  hiyo  na  tunataka kuufanya  uwe wa  haki  zaidi  na  kansela  anataka  kuufanya  uwe wa  haki  zaidi," trump  alisema.

Merkel  aliondoka  Ikulu  ya  white  House , ikionekana  kwamba hakuweza  kupata  ahadi  kutoka  kwa  Trump  kubakia katika makubaliano  ya  kinyuklia  na  Iran  ama  kupata  msamaha  wa kudumu  kwa  Ulaya   katika ushuru  wa  biashara.

Hadi  pale Trump  atakapochukua  hatua Meo  mosi, ambayo  ni Jumanne  ijayo, ushuru  katika  chuma  na  bati  kutoka  mataifa  ya Ulaya  utaanza  kutumika, huenda ukifuatiwa  na  hatua  za  kulipiza za  Umoja  wa  Ulaya  ambazo  zitazusha  vita  vya  biashara  kati  ya mataifa  ya  Ulaya  na  Marekani.

Kuhusiana  na  makubaliano  ya  kinyuklia  na  Iran, ambayo  Trump huenda  akayasambaratisha  Mei 12, Merkel alikiri  kwamba "hayajakuwa sahihi vya  kutosha" lakini  ni  muhimu  kuendelea  nayo hata  hivyo.

USA Washington | Präsident Donald Trump & Angela Merkel, Bundeskanzlerin
Trump na kansela wa Ujerumani Angela MerkelPicha: Reuters/B. Snyder

Trump alitaka  "makubaliano  hayo mabaya" ambayo  yaliipa  Tehran ahueni  ya vikwazo  ili  kuweza kuzuwia  shughuli  zake  zenye  utata za  kinyuklia, yajadiliwe  upya, jambo  ambalo  mataifa  ya  Ulaya yanaona  kuwa ni  jambo lisilokuwa  sahihi, la  hatari  na  lisilo  la lazima.

Licha  ya  kuwapo  kwa  hali  ya  kutokubaliana , Trump aligusia ukosoaji  wake  mkali  wa  matumizi  ya  chini  ya  ulinzi  ya Ujerumani , sera za  uhamiaji  za  kufungua  milango  na biashara yenye  mtazamo  wa  mauzo  ya  nje. Akimsifu Merkel  kuwa  ni "mwanamke wa aina  yake," Trump  alisisitiza "ni  lazima  tuwe  na uhusiano  wa  kibiashara  wa  haki na  unaonufaisha  pande  zote mbili kwa marafiki  zetu na  washirika wetu.

Mwandishi: Sekione  Kitojo / afpe /rtre