Merkel ataka hatua kali zaidi kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi
4 Julai 2011Matangazo
Akizungumza katika mkutano wa kimataifa kuhusu mazingira mjini Berlin, hapa Ujerumani, uliowashirikisha wawakilishi kutoka nchi 35, kansela Merkel amesema haitoshi tu, kwa nchi zenye viwanda kupunguza gesi chafu, kwa ajili ya kujaribu kupunguza ujoto duniani.
Amewaambia washiriki wa mkutano huo kwamba bado hakujapatikana makubaliano mengine yatakayoweza kuchukua nafasi ya azimio la Kyoto, ambalo linamaliza muda wake mwaka ujao.
Mkutano huo unaendelea leo, chini ya Uenyekiti wa wenyeji Ujerumani, na Afrika kusini, nchi ambayo mkutano ujao wa mabadiliko ya tabia ya nchi, unatarajiwa kufanyika.