1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Merkel ataka fursa sawa ya kibiashara na China

12 Juni 2020

Kansela Angela Merkel wa Ujerumani amesisitiza usawa kwa Ujerumani na makampuni mengine yanayofanya shughuli za kibisahra nchini China katika mazungumzo yake kwa njia ya video na Waziri Mkuu wa China Li Keqiang.

https://p.dw.com/p/3derC
Bildkombo Angela Merkel und Li Keqiang
Picha: Getty Images/AFP

Msemaji wa kansela huyo, Steffen Seibert amsema katika mazungumzo hayo ya jana Merkel ametolewa wito Li kutoa fursa ya soko bora kwa makampuni ya kigeni nchini China, ambayo ni mshirika muhimu wa kibiashara wa Ujerumani. Kansela Merkel aliweka wazi kabisa, kwamba hatua zaidi zinapaswa kuchukuliwa katika kuboresha hali ya makampuni ya kigeni nchini humo na kusisitiza umuhimu wa kuwepo kwa makubaliano ya uwekezaji kati ya Ulaya na China.

 Aidha kwa mujibu wa Seibert, Kansela Merkel alitilia mkazo pia matakwa ya Ujerumani katika kusimamia kanuni na biashara huria, kama ilivyosisitizwa katika maazimio ya Shirika la Biashara Duniani (WTO), na kuendeleza biashara madhubuti ya pamoja. Kwa mujibu wa chama cha wafanyabiashara cha Umoja wa Ulaya makampuni ya Ujerumani na Ulaya ambayo wasiwasi uliopo kwa sasa ni ongezeko la biashara zinazomilikiwa na serikali nchini China.

Mazungumzo yagusia janga la corona

Bundeswirtschaftsminister Peter Altmaier
Waziri wa Uchumi wa Ujerumani Peter AltmaierPicha: picture-alliance/dpa/A. Hoenig

Mazungumzo baina ya viongozi hao wawili, ambayo yalihudhuriwa na Waziri wa Uchumi wa Ujerumani Peter Altmaier, pia yaligusia janga la virusi vya corona na athari zake za kuuporomosha uchumi. Na hasa kujikitia katika mjadala wa kuchachua biashara baina ya mataifa hayo mawili, katika kipindi hiki cha mkwamo, na kugubikwa na uhusiano mbaya kati ya serikali za Marekani na China.

Mkutano mkubwa wa kilele kati ya Umoja wa Ulaya na China, ambao ulipaswa kufanyika mjini Leipzig nchini Ujerumani, Desemba ilisitishwa kutokana na mripuko wa janga la corona.Hata hivyo msemaji wa Merkel, Seibert amesema, miongoni mwa ajenda muhimu za Kansela Merkel katika mkutano huo na Li Keqiang ulizungumza suala la haki za binaadamu na hali ilivyo sasa mjini Hong Kong.

Kandoni mwa mkutano huo, wanasiasa kutoka katika katika kada mbalimbali walimtolewa wito Kansela Merkel kusimama kidete juu ya suala la uhuru wa Hong Kong, kwa muhtadha wa kitisho cha sheria ya usalama wa taifa ya China ambayo ilipigiwa kura mwezi Mei. Gyde Jensen, ambae ni mwenyekiti wa kamati ya bunge ya haki za binaadamu aliliambia shirika la habari la Ujerumani (DPA) wanamtarajia Merkel kulaani vikali mpango wa serikali ya China. Mwanasiasa huyo alisema  serikali ya shirikisho la Ujerumani lazima itekeleze ahadi yake ya sera za mambo ya nje ya kuzilinda haki za binaadamu.

Vyanzo DPA/DW