1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaItaly

Meloni: Italia kutoipa Ukraine ndege za kivita

22 Februari 2023

Waziri Mkuu wa Italia, Giorgia Meloni ambaye huegemea siasa kali za mrengo wa kulia, amesema suala la kuipa Ukraine ndege za kivita halipo miongoni mwa ajenda za kujadiliwa.

https://p.dw.com/p/4Nokw
Ukraine Besuch Meloni bei Selenskyj
Picha: GLEB GARANICH/REUTERS

Meloni amesema hayo baada ya kuizuru Ukraine na kuzungumza na rais wa nchi hiyo Volodymyr Zelensky.

Hata hivyo, anatafakari kuipa Ukraine mifumo zaidi ya ulinzi. Tayari nchi yake kwa ushirikiano na Ufaransa, kwa pamoja zinatuma mfumo wa ulinzi chapa SAMP/T-MAMBA

Rais Volodymyr Zelensky amekuwa akizirai nchi za Magharibi kuipa nchi yake ndege za kivita ili kupambana na kujilinda dhidi ya mashambulizi ya vikosi vya Urusi.