1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Meli ya uokoaji ya Ujerumani yawaokoa wahamiaji 100

27 Desemba 2021

Shirika la kibinafsi la uokozi wa baharini la Sea -Watch la Ujerumani, limesema kuwa limewaokoa takriban watu 100 katika bahari ya Mediterenia katika operesheni yake ya tano ndani ya siku tatu.

https://p.dw.com/p/44rfe
Deutsches Hilfsschiff Sea-Watch 4 rettet Bootsmigranten im zentralen Mittelmeer
Picha: Suzanne De Carrasco/Sea-Watch/Handout via REUTERS

Katika ujumbe kupitia mtandao wa twitter, shirika hilo limesema kuwa mwanamke mmoja mjamzito ni miongoni mwa kundi la watu waliookolewa hivi karibuni.

Wafanyakazi wa shirika hilo sasa wana takriban watu 450 waliookolewa kutoka boti za wahamiaji katika meli yao ya Sea- Watch 3.

Wakati huo huo, walinzi wa Pwani ya Italia jana waliripoti kuwa baada ya shughuli ya utafutaji ya siku mbili, walipata boti iliyokuwa imewabeba wahamiaji katika Pwani ya Crotone Kusini mwa nchi hiyo.

Katika taarifa, walinzi hao wamesema kuwa waliwaokoa watu 27 na kuwaleta katika eneo salama. Umoja wa Mataifa umesema kuwa zaidi ya watu 1500 wamefariki katika eneo la kati mwa Mediterenia mwaka huu.