1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Meli ya mwisho ya ngano yaondoka Ukraine

17 Mei 2023

Meli ya mwisho imeondoka katika bandari ya Bahari Nyeusi nchini Ukraine chini ya makubaliano yanayoikubalia Ukraine kusafirisha kwa usalama nafaka katika nchi za nje.

https://p.dw.com/p/4RUaD
Ukraine | Hafen von Odessa
Picha: Bo Amstrup/Ritzau Scanpix/AFP/Getty Images

Haya yamefanyika siku moja kabla Urusi kujiondoa kutoka kwenye makubaliano hayo kutokana na vikwazo vilivyoko katika mauzo yake ya nafaka na mbolea nje ya nchi.

Kulingana na taarifa ya Umoja wa Mataifa, meli hiyo DSM Capella, imeondoka katika bandari ya Chornomorsk ikiwa imebeba tani 30,000 za mahindi na inaelekea Uturuki.

Mnamo mwezi Novemba, Urusi ilikubali kurefusha muda wa makubaliano hayo ya kusafirisha nafaka ya Bahari Nyeusi kwa siku 120 ila mnamo mwezi Machi, ikakubali kurefusha muda huo kwa siku 60 hadi Mei 18, hadi pale orodha ya matakwa yake kuhusiana na mauzo ya mavuno yake yatakapotimizwa.