1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Meli ya Mafuta ya Iran yaelekea Ugiriki kutoka Gibralter

Oumilkheir Hamidou
19 Agosti 2019

Meli ya mafuta ya Iran iko njiani kuelekea Ugiriki baada ya kuruhusiwa kung'owa nanga kisiwani Gibralter. Viongozi wa mjini Teheran wameonya hatua yoyote ya Marekani ya kuizuwia meli hiyo itakuwa na "madhara makubwa:"

https://p.dw.com/p/3O7FT
Öltanker Adrian Darya -  Grace 1 bei Nacht
Picha: Reuters/J. Nazca

Meli hiyo iliyobadilishwa jina hivi sasa na kuitwa Adria Darya nambari moja badala ya Greece nambari moja imeng'owa nanga Gibralter saa tano za usiku jana. Ratiba ya safari inaonyesha meli hiyo inaelekea Kalamata nchini Ugiriki . Inatarajiwa kuwasili huko jumaapili inayokuja. Balozi wa Iran nchini Uingereza Hamid Baeidinejad amethibitisha kupitia mtandao wa instagram mapema  kwamba meli hiyo "imeshaondoka Gibralter baada ya kuzuwiliwa kwa siku 45."

Meli Adrian Darya yaelekea katika bahari ya Mediterenia
Meli Adrian Darya yaelekea katika bahari ya MeditereniaPicha: Getty Images/AFP/J. Guerrero

Gibralter yaruhusu meli ya mafuta ya Iran ing'owe nanga

Meli  ya mafuta ya Iran ilikamatwa na jeshi la wanamaji la Uingereza julai 4 iliyopita kwa tuhuma za kusafirisha mafuta hadi Syria kinyume na vikwazo vya Umoja wa ulaya. Kisa hicho kilizusha mvutano uliodumu wiki kadhaa kati ya Teheran na nchi za magharibi. Kimezidisha makali pia ya mvutano katika njia za kimataifa za kusafirishia mafuta katika Ghuba.

Gibralter, eneo linalodhibitiwa na Uingereza ilibatilisha amri ya kuzuwiliwa meli hiyo alkhamisi iliyopita lakini  siku ya pili yake korti kuu ya mjini Washington ikachapisha waranti kutaka meli hiyo izuwiliwe. Maafisa wa Gibralter wamesema hawawezi kutekeleza matakwa hayo kwasababu wanalazimika kufuata asheria za Umoja wa ulaya.Washington inataka meli hiyo izuwiliwe kwa hoja za kuwepo mafungamano pamoja na tume ya walinzi wa mapinduzi ya kiislam ambayo Marekani inawataja kuwa magaidi.

Kiongozi mkuu wa kidini Ayatollah Ali Khamenei
Kiongozi mkuu wa kidini Ayatollah Ali KhameneiPicha: picture-alliance/abaca/Parspix

Iran inaonya dhidi ya meli yake kuzuwiliwa tena na Marekani

Viongozi wa Ugiriki hawakusema chochote kuhusiana na mvutano huo. Akiulizwa kama Marekani inaweza kutoa tena maombi ili meli hiyo ikamatwe, msemaji wa wizara ya mambo ya nchi za nje ya Iran. Abbas Mousavi amesema tunanukuu:"Hatua kama hiyo na pia  mjadala kuhusu suala hilo yatahatarisha usalama wa safari za meli baharini. Akizungumza kupitia televisheni ya taifa, Musavi amesema Iran imetuma onyo kupitia njia rasmi na hasa kwa ubalozi wa Uswisi, na maafisa wa Marekani wasifanye makosa kama hayo kwasababau anasema "matokeo yake yatakuwa mabaya."

Itafaa kusemam hapa kwamba Uswisi ndiyo inayowakilisha masilahi ya Marekani nchini Iran.

 

Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/Reuters/AFP/dpa

Mhariri: Mohammed Khelef