1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Melania Trump aunga mkono haki ya kutoa mimba

4 Oktoba 2024

Mke wa Donald Trump, Melania Trump, anaunga mkono haki ya kutoa mimba katika kumbukumbu yake aliyoiandika, msimamo ambao ni kinyume na mumewe ambaye ni mgombea wa urais wa Marekani kwa tiketi ya chama cha Republican.

https://p.dw.com/p/4lP8N
Melania Trump
Mke wa rais wa zamani wa Marekani, Melania Trump.Picha: Leon Neal/Getty Images

Suala hilo ni mojawapo wa mambo nyeti lenye kugawa pande tofauti katika uchaguzi ujao.

Kulingana na dondoo kutoka kwenye kitabu chake hicho cha kumbukumbu, Melania ameandika kwamba "ni muhimu kuhakikisha kwamba wanawake wana uhuru katika kuamua kuwa na watoto kutokana na hali zao, bila kuingiliwa au kupata shinikizo kutoka kwa serikali."

Soma zaidi: Trump na mkewe waambukizwa virusi vya corona

Msimamo huu wa Melania, unatofautiana na ule wa mumewe Trump ambaye mara kwa mara hujipiga kifua kwamba mahakimu aliowachagua kuiongoza Mahakama Kuu nchini humo, walisafisha njia ya kufikisha mwisho haki ya kitaifa ya uavyaji mimba.

Timu ya kampeni ya mpinzani wa Trump, makamu wa rais Kamala Harris, imeitumia tofauti hiyo ya wazi kati ya Trump na mkewe kuhusiana na suala hilo kwa ajili ya kuvutia upande wao. Harris anaunga mkono uavyaji mimba.