1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kenya: Mchungaji mwingine wa kanisa la New Life akamatwa

28 Aprili 2023

Waendesha Mashtaka nchini Kenya wamesema watamfungulia kesi ya "mauaji ya halaiki" kiongozi mwingine wa kanisa aliyekamatwa jana kwa madai ya kusababisha vifo vya idadi kubwa ya wafuasi wake.

https://p.dw.com/p/4QfCZ
Polizisten eskortieren Ezekiel Ombok Odero im Polizeipräsidium in Mombasa
Picha: Stringer/REUTERS

Ezekiel Odero, mchungaji wa kanisa la New Life Prayer Centre alikamatwa ikiwani ni siku chache baada ya mchungaji Paul Mackenzie kukamatwa kwa kusababisha vifo vya waumini wake aliyowashawishi kuacha kula na kunywa ile wafike mbinguni.

Katika msako uliofanikisha kukamatwa kwake, waziri wa mambo ya ndani wa Kenya Kithure Kindiki amesema mamlaka zimefanikiwa kuwaondoa zaidi ya watu 100 waliokuwa wakizuiwa kwenye kanisa la mchungaji huyo.

Soma pia: Uchunguzi wa maiti za maafa ya msitu wa Shakahola waanza

Afisa wa eneo hilo Rhoda Onyancha amesema kukamatwa kwa mchungaji Ezekiel kunafuatia madai ya vifo vinavyotokea kwenye eneo lake vilivyoripotiwa kwenye baadhi ya vyumba vya kuhifadhia maiti na taasisi mbalimbali.