1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mbinu ya kuelekea Mashariki ya Kazi

Maja Dreyer19 Juni 2007

Suala la kwanza lililozingatiwa katika uchambuzi wa leo ni hali ya kisiasa katika maeneo ya Wapalestina, hususan serikali mpya ya rais Mahmud Abbas.

https://p.dw.com/p/CHSf

Likitathmini matokeo haya, gazeti la “Kölner Stadtanzeiger” limeandika:

“Suala la Wapalestina linaonekana kama limegawanyika katika pande mbili: mmoja mzuri na mwingine mbaya. Bila ya kupoteza muda, kundi la pande nne zinazoshughulikia suala la Mashariki ya Kati limemuunga mkono rais Abbas na serikali yake ya dharura. Umoja wa Ulaya pia uko tayari tena kutoa msaada wa kifedha. Na Israel inapanga kulipa kiwango kikubwa cha malipo ya forodha na kodi kwa Wapalestina yaliyozuiliwa kwa muda wa mwaka mmoja na nusu. Gaza lakini, kwa upande mwingine, haitapata msaada, ila tu juhudi za kuzuia janga la binadamu. Lengo la mbinu huu ni wazi: Wapalestina wanatakiwa wafahamu kuwa maisha ni bora chini ya mamlaka ya chama cha Fatah na siyo chini ya Hamas wenye msimamo mkali.”

Ni uchambuzi wa “Kölner Stadtanzeiger”. Mhariri wa gazeti la “Financial Times Deutschland” lakini hafahamu mbinu ya Umoja wa Ulaya na anauliza:

“Umoja wa Ulaya una lengo gani? Je, unataka kumpa nguvu rais Abbas pamoja na chama chake cha Fatah ili aweze kulilipa kisasi dhidi ya kundi la Hamas katika ukanda wa Gaza? Labda unasubiri tu hadi suala la taifa la Hamas litakapojiondosha lenyewe – au litatatuliwa na jeshi la Israel? Umoja wa Ulaya unapaswa kutafuta njia vipi unaweza kushughulikia pande zote mbili za Wapalestina. Hakuna mtu yeyote anayetaka mamlaka ya Wapalestina yavunjike haraka.”

Na suala la pili ambalo linaendelea kuzusha mivutano ndani ya Umoja wa Ulaya ni upinzani wa Poland dhidi ya katiba mpya ya Umoja huu, ikipinga hasa mfumo mpya wa kupiga kura. Kwa maoni ya mhariri wa “Fuldaer Zeitung”, takwa la Poland kuwa na usemi mkubwa kama ule wa Ujerumani ni la kifidhuli. Ameandika:
“Ujerumani inachangia kwa kiwango kikubwa zaidi ndani ya Umoja wa Ulaya. Poland, lakini, iko upande mwingine, yaani inapata msaada mkubwa zaidi kutoka kwa Umoja huu. Licha ya msaada huu, nchi hii inafanya kama itakavyo na pia inazilazimisha nchi nyingine wanachama kukubali takwa lake. Hivyo lakini, Poland imejitenga na Umoja huu.”

Mhariri wa “Westdeutsche Zeitung” ana maoni haya haya na anaongeza kusema:

“Yule aliyetaka kupatiwa ushahidi, kwa nini Umoja wa Ulaya unahitaji mfumo wa kura nyingi, ili uweze kuendelea kufanya kazi, basi ushahidi amepatiwa na Poland.”

Na hatimaye tunalinukuu gazeti la “Saarbrücker Zeitung” na shauri lake kwa Poland:

“Viongozi hao wa Poland, huenda hawajafahamu somo muhimu juu ya jumuiya ya Ulaya: Yaani yule tu anayeimarisha Umoja, ataongeza pia umuhimu wake ndani ya Umoja huu. Wafahamu kuwa hawawezi hauzuia Umoja wa Ulaya, lakini bado wana fursa ya kuunganishwa. Lakini wakiendelea na mbinu hii ya upinzani, watajiweka kandoni.”