1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MAZUNGUMZO MALAWI YAVUNJIKA

22 Februari 2005
https://p.dw.com/p/CFbp

BLANTYRE:

Mazungumzo baina ya rais wa Malawi Bingu wa Mutharika na vikundi kadhaa vya upinzani nchini ili kuunda chama kipya cha kisiasa yameshindwa kufaulu . Wa Mutharika amejiuzulu kutoka chama cha United Democratic Front (UDF) mapema mwezi huu ili kuzima changamoto kutoka rais aliemtanguliwa Bakili Muluzi. Wa Mtharika amekuwa akijadiliana na na chama cha Republican party –muungano wa vyama 4 vidogo pamoja na Movement for Democratic change ,lakini vikundi hivyo vimearifu leo kwamba mazungumzo yaizika.