1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi: Mazugumzo ya kubadilishana wafungwa yako njia panda

22 Desemba 2023

Naibu waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Ryabkov amesema mazungumzo na Marekani juu ya uwezekano wa kubadilishana wafungwa yanatatizwa na kumulikwa na vyombo vya habari na matakwa yasio ya kawaida ya Marekani

https://p.dw.com/p/4aUoA
Sergei Alexejewitsch Rjabkow | stellvertretender russischer Außenminister
Picha: Joe Klamar/AFP/Getty Images

Mazungumzo hayo yananuia kutoa fursa ya kuachiliwa huru kwa Wamarekani wanaoshikiliwa nchini Urusi.Wiki iliyopita, wizara ya mambo ya nje ya Marekani ilieleza kuwa Urusi imekataa mapendekezo kadhaa ya kuwaachilia Paul Whelan, Mmarekani anayetuhumiwa kwa ujasusi na mwandishi wa jarida la Wall Street , Evan Gershkovich, ambaye amezuiliwa tangu mwezi Machi na anayekabiliwa pia na mashtaka ya ujasusi.Marekani imeeleza kuwa,wawilihao walikamatwa kimakosa na kwamba kesi dhidi yao imeangaziwa kupita kiasi na vyombo vya habari. Rais wa Urusi Vladimir Putin alisema wiki iliyopita kwamba Moscow inajadiliana na Marekani juu ya kadhia ya wawili hao, na kwamba ikulu ya Kremlin inatarajia "kupata suluhu."