1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mazingira ya kazi kwa wanaharakati Tanzania ni magumu, HRW

Mwandishi: Hawa Bihoga DW/Dar es salaam (Mhariri: 28 Aprili 2020

Mtandao wa watetezi wa haki za binaadamu nchini Tanzania umesema katika mwaka 2019, watetezi wa haki za binadamu nchini humo walifanya kazi za utetezi katika mazingira magumu zaidi.

https://p.dw.com/p/3bWQi
Tansania Daressalam Polizeieinsatz nach Gerichtsurteil
Picha: DW/S. Khamis

Kulingana na ripoti wa shirika la Human Rights Watch kuhusu hali ya haki za binadamu mwaka uliopita, miongoni mwa wanaharakati walifunguliwa kesi za kimkakati pamoja na vitendo 71 vya uvunjifu wa haki zao. 

Katika ripoti hiyo ya saba kutolewa Mtandao wa watetezi wa haki za binadamu THRDC umezitaja kwa kina kesi tisa za kimkakati zilizofunguliwa mwaka 2019 kama miongoni mwa vielelezo pamoja na matendo 71 dhidi ya watetezi wa haki za binaadamu.

Vitendo vya ukiukwaji wa sheria pamoja na haki za binaadamu ikiwemo kukamatwa kinyume cha sheria, vitisho, uminywaji wa uhuru wa kujieleza pamoja na kufunguliwa kesi zisizo na msingi, yametajwa kwenye ripoti kuwasakama watetezi huku baadhi ya wahusika wa vitendo hivyo ni vyombo vya dola na watu binafsi.

Onesmo Ole Ngurumwa mratibu wa mtandao huo amesema kuwa, matendo hayo ya ukiukwaji wa haki kwa kundi hilo muhimu kwenye jamii yameonekana kuongezeka huku baadhi ya sheria zinaonekana kutoa mwanya kwa kwa watetezi kurudi nyuma katika kutekeleza majukumu yao:

Waandishi habari Tanzania wapitia unyanyasaji

Baadhi ya vyombo vya habari Tanzania vimetozwa faini au kufungwa, waandishi wamenyang'anywa vitendea kazi na kusimamishwa.
Baadhi ya vyombo vya habari Tanzania vimetozwa faini au kufungwa, waandishi wamenyang'anywa vitendea kazi na kusimamishwa.Picha: DW/S. Khamis

Ripoti hiyo inaonesha jinsi waandishi wa habari hapa nchini wanavyopitia unyanyasaji mkubwa wakati wakitekeleza majukumu yao, kutozwa faini kwa vyombo vya habari bila kuzingatia taratibu, kunyang'anywa vitendea kazi na kusimamishwa au kufungiwa kwa baadhi ya vyombo vya habari. Jumla ya matukio 36 ya aina hiyo imeripotiwa, idadi ambayo imepiku miaka iliopita.

Kwa upande wake, nazo asasi za kiraia zinaonekana kuathirika pakubwa kutokana na sheria kandamizi ambazo zinatoa mamlaka makubwa kwa msajili, ambapo katika kipindi hicho Mashirika yasiyo ya Kiserikali yapatayo 158 yalifutiwa usajili kwa kile kilichotajwa kutokuzingatia masharti ya Sheria ya Mashirika yasiyo ya Kiserikali marekebisho ya mwaka 2019:

Mtandao huo umeitaka serikali kutambua kazi za watetezi kwa kutengeneza mazingira wezeshi, kurekebisha Sheria walizozitaja si rafiki katika utendaji kazi, zikiwemo Sheria ya Makosa ya Mtandao 2015, Sheria ya Vyombo vya Habari 2016 na Kanuni za Maudhui Mtandaoni 2018 ili kustawisha utendaji kazi wa watetezi wa haki za binadamu nchini.