1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mawaziri wa EU waridhia kuleta mageuzi ya sheria za madeni

21 Desemba 2023

Mawaziri wa fedha wa nchi za Umoja wa Ulaya wamefikia mapatano juu ya mageuzi ya sheria za madeni baada ya juhudi za miezi kadhaa.

https://p.dw.com/p/4aSEs
Uholanzi l Waziri wa fedha wa Uholanzi Sigrid Kaag
Waziri wa fedha wa Uholanzi Sigrid KaagPicha: Sem Van Der Wal/ANP/dpa/picture alliance

Mageuzi hayo yatazipa nchi za Umoja huo  zenye madeni makubwa, muda wa kutosha wa kupunguza nakisi na pia yatazipa wigo mpana zaidi wa kuwekeza.

Mnamo miaka ya karibuni madeni yalifikia viwango vya kuvunja rekodi katika nchi hizo, kutokana na janga corona na pia kutokana na juhudi za kupambana na bei za juu za nishati zilizosababishwa na vita vya Ukraine.

Waziri wa fedha wa Uholanzi Sigrid Kaag, amesema pana motisha ya kuleta mageuzi na fursa ya kuwekeza.

Amesema  sheria husika zitawekwa kwa usahihi zaidi kulingana na  mahitaji.