1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa video kuhusu corona kufanyika Ulaya

6 Aprili 2020

Mawaziri wa ulinzi na sheria wa Umoja wa Ulaya watafanya mikutano kadhaa kupitia kanda za video leo, wote wakijikita katika madhara ya ugonjwa wa Covid-19 Ulaya.

https://p.dw.com/p/3aVXx
Coronavirus - Sitzung des EU-Parlaments in Brüssel
Picha: AFP/K. Tribouillard

Mawaziri wa sheria watazungumzia hatua mpya za kisheria zilizoc (SW): Mawaziri wa ulin... hukuliwa kukabiliana na janga hili na pia kuhusu hali ilivyo katika magereza kutokana na mripuko huo.

Mawaziri hao bila shaka pia watazungumzia hali ilivyo nchini Hungary ambapo jawabu la nchi hiyo kwa janga la virusi vya corona limeshuhudia Waziri Mkuu Viktor Orban kupewa mamlaka makubwa bila kikomo.

Hungary imeghadhabishwa na shutuma kutoka kwa nchi za Umoja wa Ulaya kuhusiana na hatua yake hiyo kwa kusema ni jambo litakalosaidia kupambana na mripuko wa virusi vya corona.

Wakati huo huo mawaziri wa ulinzi wanatarajiwa kujadili kile kinachofanywa na majeshi kusaidia kukabiliana na kusambaa kwa virusi hivyo.