1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaPeru

Mawaziri wa mataifa manne Amerika ya Kusini kujadili usalama

16 Januari 2024

Mawaziri wa mambo ya kigeni, ulinzi na wa mambo ya ndani wa mataifa manne ya Amerika ya Kusini watakutana kujadili tatizo la biashara haramu ya dawa za kulevya iliyoitumbukiza kanda hiyo kwenye mzozo wa kiusalama.

https://p.dw.com/p/4bHmg
Udhibiti wa uhalifu nchini Ecuador
Uhalifu unaohusishwa na magenge ya wahuni yanayofadhiliwa kupitia biashara ya dawa za kulevya umeyatikisa mataifa ya Amerika ya Kusini hususani Ecuador. Picha: AFP/Getty Images

Tangazo kuhusu mkutano huo wa mwishoni mwa juma hilo limetolewa na waziri mkuu wa Peru, Alberto Otarola, alipozungumza na waandishi habari  jana jioni.

Amesema mkutano huo utafanyika kwenye mji mkuu wa nchi hiyo, Lima, mnamo Jumapili inayokuja na utawaleta pamoja mawaziri wa Peru, Bolivia, Colombia na Ecuador

Otarola amesema ni muhimu kwa nchi hizo nne kukomesha biashara ya dawa za kulevya inayovuka mipaka, ambayo "ndiyo inafadhili shughuli za magenge ya uhalifu yanayosababisha vurugu, mauaji na wasiwasi ikiwemo vurumai iliyoshuhudiwa hivi karibuni nchini Ecuador."

Mkutano huo utajadili njia za kubadilishana taarifa za kijasusi pamoja na ushirikiano zaidi baina ya vyombo vya usalama vya mataifa hayo jirani.