1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Mawaziri wa nje wa Ulaya waonyesha mshikamano na Ukraine

2 Oktoba 2023

Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell amesema mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja huo wanakutana mjini Kiev kama ishara ya kuiunga mkono Ukraine.

https://p.dw.com/p/4X2hg
Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell akizungumza mjini Brussels, Julai 20, 2023
Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell akizungumza mjini Brussels, Julai 20, 2023Picha: Sierakowski/EUC/ROPI/picture alliance

Mkuu huyo wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell aidha amesema mustakabali wa Ukraine upo mikononi mwa Umoja huo wa Ulaya.

Huo ni mkutano wa kwanza wa ngazi ya mawaziri kufanyika kwenye ardhi ya nchi isiyo mwanachama wa Umoja wa Ulaya.

Waziri wa masuala ya kigeni wa Ukraine Dmytro Kuleba amesema mkutano huo unatuma ujumbe kwamba Umoja wa Ulaya unatanuka kuingia Ukraine. Mkutano huo haukutangazwa hapo kabla kutokana na sababu za kiusalama.

Moja ya ajenda ya majadiliano ni pendekezo la Borrell, la kurefusha muda wa kujitolea kuifadhili Ukraine kwa kuipa silaha  na pia kutumia fedha za Umoja wa Ulaya kutoa ndege za kisasa za kivita na makombora kwa Ukraine.