1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mawaziri wa EU kujadili tena mageuzi ya uombaji hifadhi

28 Septemba 2023

Mawaziri wa mambo ya ndani wa nchi za Umoja wa Ulaya wanatarajiwa kukutana leo mjini Brussels Ubelgiji kujaribu kupiga hatua kuhusu suala tete la mageuzi ya mfumo wa Umoja wa Ulaya kuhusu waomba hifadhi.

https://p.dw.com/p/4WuMZ
Mawaziri wa ndani wa Eu wakutana Brussels kuhusu uhamiaji
Mawaziri wa ndani wa Eu wakutana Brussels kuhusu uhamiajiPicha: KENZO TRIBOUILLARD/AFP

Mawaziri wa mambo ya ndani wa nchi za Umoja wa Ulaya wanatarajiwa kukutana leo mjini Brussels Ubelgiji kujaribu kupiga hatua kuhusu suala tete la mageuzi ya mfumo wa Umoja wa Ulaya kuhusu waomba hifadhi.

Idadi ya wahamiaji wanaofika katika Umoja wa Ulaya imeongezeka mno katika miezi ya hivi karibuni, na kufichua mivutano ambayo haijatatuliwa kuhusu suala hilo kati ya nchi 27 wanachama wa umoja huo.

Kipengee kimoja kinachojadiliwa sasa na ambacho kimezusha mvutano mkubwa ni cha udhibiti wa mgogoro panapotokea wimbi kubwa la wahamiaji.

Pendekezo la mwezi Julai halikuweza kuwashawishi walio na msimamo mkali na vilevile serikali ya Ujerumani kwa sababu mbalimbali na kusababisha mkwamo.

Makubaliano kwenye mkutano huo yatategemea pakubwa ikiwa Ujerumani itakuwa tayari kubadili msimamo wake ili kutatua mkwamo uliopo.