1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Mawakili wa Imran Khan kukutana naye baada ya hukumu ya jela

7 Agosti 2023

Mawakili wa waziri mkuu wa zamani wa Pakistan, Imran Khan, wataruhusiwa kukutana na mwanasiasa huyo baadaye leo kabla ya kukata rufaa dhidi ya uamuzi uliomtia hatiani na kuhukumiwa kifungo cha miaka mitatu gerezani.

https://p.dw.com/p/4Ur53
Pakistans ehemaliger Premierminister Imran Khan
Picha: Mohsin Raza/REUTERS

Mmoja ya wanasheria wanaomwakilisha, Naeem Panjhuta, amesema mamlaka za magereza nchini humo zimewapatia nafasi ya kukutana na Khan katika jela ya wilaya ya Attock alikopelekwa Jumamosi baada ya mahakama kutoa hukumu. 

Amesema pia wameanza matayarisho ya kukata rufaa dhidi ya hukumu iliyomtia hatiani mwanasiasa huyo kwa makosa ya ufisadi unaohusu  kuuza zawadi za serikali alizopewa akiwa madarakani. 

Soma zaidi: Waziri Mkuu wa zamani wa Pakistan ahukumiwa miaka 3 jela

Khan, mwenye umri wa miaka 70, amekuwa katikati ya msukusuko wa kisiasa tangu alipotolewa madarakani kama waziri mkuu mwaka uliopita kupitia kura ya kutokuwa na imani.

Mwenyewe analituhumu jeshi na wapinzani wake kisiasa kwa kula njama dhidi yake kupitia njia za kisheria.