1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mauaji ya kiholela na watu kutoroshwa Kenya, wanaharakati

Faiz Musa31 Agosti 2020

Mashirika ya kutetea haki za kijamii Kenya yasema watu wapatao 100 hawajulikani walipo baada ya kutekwa. Wengine wamepatikana wameuawa kwa njia za kikatili katika Pwani ya Kenya katika kipindi cha miaka mitatu sasa.

https://p.dw.com/p/3hnl0
Picha ya maktaba (11.09.2016): Maafisa wa polisi wakifika katika kituo cha polisi cha Central Mombasa ambapo wanawake watatu walipigwa risasi baada ya kudaiwa kujaribu kufanya shambulizi kutumia bomu la petroli.
Picha ya maktaba (11.09.2016): Maafisa wa polisi wakifika katika kituo cha polisi cha Central Mombasa ambapo wanawake watatu walipigwa risasi baada ya kudaiwa kujaribu kufanya shambulizi kutumia bomu la petroli.Picha: picture-alliance/dpa

Watetezi wa haki za kibinadamu nchini Kenya kupitia shirika la kutetea haki za binadamu la Haki Afrika wameitoa ripoti yao inayodai kwamba serikali ya Kenya inahusika katika visa hivyo.

Mashirika hayo yanaeleza kwamba licha ya juhudi mbali mbali zinazofanywa na watetezi wa haki za binadamu kupitia mahakama na hata kushiriki maandamano ya mara kwa mara visa hivyo bado vinaendelea kuripotiwa hasa Mombasa, Kwale, Lamu, Kilifi na Tana River.  Yanasema kuwa matukio hayo yanahusiana na harakati za serikali katika kukabiliana na ugaidi.

Mashirika hayo sasa yamewasilisha hati ya malalamishi yao katika idara ya polisi katika kaunti ya Kwale wakitaka serikali kujitokeza na kuwajibika katika masuala hayo ya ukiukaji wa haki za binadamu.

Mkuu wa kituo cha polisi eneo la Diani kaunti ya Kwale Nehemiah Bito amepokea hati hiyo hizo na kuahidi kwamba serikali itashughulikia mapendekezo yaliyomo.