1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Matumaini ya muwafaka kati ya India na Pakistan

4 Januari 2004
https://p.dw.com/p/CFmD
ISLAMABAD: Wakitoa mwito wa masikizano na ushirikiano, katika mkutano wa kilele wa nchi za Asia ya Kusini mjini Islamabad viongozi wa serikali za India na Pakistan wameleta matumaini kuwa madola hayo mawili yanaweza yakafikia muwafaka. Matumaini yalikuwa juu viongozi hao wawili Atal Bihari Vajpayee na Zafarullah Jamali walipokutana nje ya vikao rasmi. Ulikuwa mkutano wa kwanza kati ya wanasiasa hao wawili. Lakini kiini hasa cha mkutano huo wa siku tatu kinahusika na zile juhudi za kufanyika mkataba kuhusu eneo huru la kibiashara kati ya nchi saba zanachama ambazo kwa pamoja yana kadiri asili miya 20 ya wakazi wa dunia na kadiri nusu ya masikini wa dunia. Wanachama wa Jumuiya ya Nchi za Asia ya Kusini (SAARC) ni India, Pakistan, Bangladesh, Bhutan, Sri Lanka na Maldives.