1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIsrael

Mateka wa Israel waliouawa Gaza walikuwa na bendera nyeupe

16 Desemba 2023

Mateka watatu wa Israeli waliouawa kimakosa na vikosi vya Israel katika Ukanda wa Gaza walikuwa wamebeba bendera nyeupe.

https://p.dw.com/p/4aFfU
Kikosi cha wanajeshi wa Israel wakimsikiza kamanda wao kabla kuingia katika ukanda wa Gaza mnamo Desemba 13, 2023
Kikosi cha wanajeshi wa IsraelPicha: Ohad Zwigenberg/AP/picture alliance

Afisa huyo amesema kuwa mwanajeshi mmoja aliwaona mateka hao wakitokea umbali wa mita kadhaa kutoka eneo walipokuwa wanajeshi hao wa Israel hapo jana katika mji wa Shejaiya, eneo la mapigano makali Kaskazini mwa Gaza wakiwa wamevalia nguo za raia na pia kutumia mbinu nyingine za kuhadaa.

Soma pia:Wanajeshi wa Israel wahimizwa kuwa waangalifu zaidi baada ya kuuawa kwa mateka

Akizungumza na wanahabari kwa njia ya simu, afisa huyo amesema kuwa mateka hao hawakuwa wamevalia mashati na pia walikuwa wamebeba fimbo zilizokuwa zimefungwa kitambaa cheupe, hali iliyowafanya wanajeshi hao kuingia uoga na kufyatua risasi. Mateka wawili waliuawa papo hapo .

Hatua ya wanajeshi wa Israel ilikuwa kinyume che sheria

Mateka wa tatu alijeruhiwa na kuingia katika jengo moja ambapo alitoa wito wa msaada kwa kiebrania na haraka kiongozi wa kikosi hicho akatoa amri ya kusitishwa kwa shambulizi hilo, lakini risasi ikafyatuliwa tena kueleka kwa mateka huyo na kumuuwa.

Afisa huyo anasema hatua hiyo ilikuwa kinyume cha sheria zao.