1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yakasirishwa na matamshi ya Waziri Mkuu wa Uhispania

30 Novemba 2023

Israel imemuita balozi wa Uhispania nchini humo kutoa malalamiko yake na kumrejesha nyumbani balozi wake mjini Madeid, baada ya waziri mkuu wa Uhispania kusema anashuku iwapo nchi inaheshimu sheria ya kibinadamu Gaza.

https://p.dw.com/p/4Zcuj
Spanien | Vereidigung Pedro Sanchez in Madrid
Picha: Manu Fernandez/AP Photo/picture alliance

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema alimuagiza waziri wake wa mambo ya nje, Eli Cohen, kumwita balozi wa Uhispania ili kutoa karipio "baada ya kauli ya aibu ya waziri mkuu wa Uhispania katika siku ambayo magaidi wa Hamas wanawaua Waisraeli katika mji mkuu wetu Jerusalem".

Wapiganaji wawili wa kundi la Hamas waliwauwa raia watatu katika kituo cha mabasi cha Jerusalem wakati wa asubuhi siku ya Alhamisi.

Soma pia: Israel na Hamas waendelea kubadilishana mateka na wafungwa

Kundi lhilo la Palestina lina ngome yake katika Ukanda wa Gaza, ambako lilianzisha mashambulio ya Oktoba 7 nchini Israel, na kusababisha vita.

Katika chapisho la mtandao wa kijamii, Cohen alisema balozi wa Israel nchini Uhispania alikuwa ameitwa nyumbani kwa mashauriano.

"Israel inajiendesha na itaendelea kujiendesha kwa mujibu wa sheria za kimataifa," Cohen alisema.