1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mataifa ya G7 yatakiwa kuzisaidia nchi masikini

24 Juni 2022

Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu, Amnesty International, limetoa wito kwa kundi la mataifa saba yaliyoendelea zaidi kiviwanda G7, kutoa msaada kwa mataifa maskini.

https://p.dw.com/p/4DD8n
Symbolbild | Deutschland | G7 Gipfel
Picha: Janine Schmitz/photothek/picture alliance

Misaada hiyo itasaidia kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa. Wito huo umetolewa kabla ya kuanza kwa mkutano wa kilele wa G7 utakaofanyika Jumapili nchini Ujerumani.

"Tunatoa wito kwa mataifa ya G7, kuwajibika kwa vitendo," amesemwa Annelen Micus, mtaalam wa hali ya hewa na haki za binadamu wa Shirika la Amnesty nchini Ujerumani.

Aliongezea kusema kuwa "kulinda haki za makundi yaliyotengwa kimaendeleo na walioathirika na mabadiliko ya hali ya hewa lazima izingatiwe kwenye sera ya hali ya hewa. Ujerumani ndiyo raisi wa G7, hivyo ina nafasi kubwa ya kulinda haki za binadamu, na izingatie mabadiliko ya hali ya hewa.

"Serikali ya Ujerumani inapaswa kuweka uzito zaidi, kwa kufadhili fedha ili kuwapa fidia wale ambao haki zao za binadamu zimejeruhiwa na uharibifu au hasara zinazosababishwa na mabadiliko ya hali ya hewa,” alisema.

Wakuu wa mataifa ya G7 watakutana huko Bavaria kuanzia Juni 26 hadi 28. Agenda mojawapo ni mapambano ya kimataifa dhidi ya mabadiliko ya hali ya hewa.

"Mafanikio ya G7 unategemea kuhusu kama wataweza kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa. Pia alisema kuwa, hatua katika kukabiliana na uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine haikuweza kuruhusiwa  juhudi za kusimamia mabadiliko ya hali ya hewa kwaani juhudi hizo ni pamoja na mabadiliko ya kimataifa kutafuta nishati mbadala,'' alifafanua Christiane Averbeck, mkurugenzi wa shirika la hali ya hewa la Ujerumani.

(dpa)