1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UchumiAfrika

Mataifa manne ya Afrika Mashariki yawasilisha bajeti 2024/25

14 Juni 2024

Mataifa manne ya Afrika Mashariki hapo jana yaliwasilisha bungeni bajeti za mwaka wa fedha unaokuja chini ya kiwingu cha ongezeko la madeni, bei kubwa za nishati na kuuanguka kwa thamani ya kipato cha mtu mmoja mmoja.

https://p.dw.com/p/4h15U
MWIGULU NCHEMBA
Waziri wa Fedha wa Tanzania, Mwigulu Nchemba.Picha: Deo kaji Makomba/DW

Nchini Kenya Waziri wa Fedha Njuguna Ndung'u aliwasilisha makadirio ya bajeti ya kiasi shilingi Trilioni 4 inayojumuisha mapendekezo ya nyongeza ya kodi na ushuru ambayo wakosoaji wanasema yatazidisha mzigo kwa raia wa kawaida.

Serikali ya Tanzania yenyewe imependekeza makadirio ya shilingi trilioni 44.39 kwa ujao wa fedha huku Bunge la Uganda tayari limeidhinisha bajeti ya shilingi trilioni 72.13 iliyosomwa jana. Rwanda nayo iliweka mezani bajeti ya kiasi faranga Trilioni 5.69 ikiwa ni nyongeza ya asilimia 11.2 ikilinganishwa na ya mwaka uliopita.

Benki ya Maendeleo ya Afrika inakadiria uchumi wa kanda ya Afrika Mashariki utakua hadi kufikia asilimia 5.7 mwaka ujao hali inayoleta matumaini baada ya kipindi cha ukuaji duni wa uchumi.