1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mataifa makubwa yakubali mpango wa mpito Syria

Sekione Kitojo1 Julai 2012

Mataifa makubwa duniani yamekubaliana Jumamosi (30.06.2012) kuhusu mpango wa mpito nchini Syria ambao unaweza kujumuisha maafisa wa serikali iliyopo madarakani, lakini rais Assad hatahusika katika serikali hiyo.

https://p.dw.com/p/15Ooa
epa03289048 Kofi Annan (C), Joint Special Envoy of the United Nations and the Arab League for Syria, arrives for a meeting of the Action Group for Syria at the European headquarters of the United Nations in Geneva, Switzerland, 30 June 2012. The Action Group are meeting to map out ways to end the ongoing bloodshed in the unrest-hit Middle East nation. EPA/MARTIAL TREZZINI
Kofi Annan katika mkutano wa Geneva kuhusu SyriaPicha: picture-alliance/dpa

Urusi na China zimesisitiza kuwa Wasyria wanapaswa kuamua juu ya vipi kipindi hicho cha mpito kitafanyika badala ya kuruhusu watu wengine kuamua hatima ya nchi hiyo kwa niaba yao, wakati mataifa hayo mawili yenye ushawishi mkubwa yakitia saini makubaliano ya mwisho ambayo hayakutoa wito wowote wa moja kwa moja kwa Assad kuachia madaraka.

Makubaliano hayo yamekuja licha ya shaka shaka za mwanzo kutoka kwa washiriki juu ya uwezekano wac mazungumzo ya Geneva huku kukiwa na mgawanyiko mkubwa kati ya mataifa ya magharibi kwa upande mmoja na China na Urusi kwa upande mwingine juu ya kumaliza kwa ghasia na matumzi ya nguvu ambayo yamesababisha kiasi watu 83 kupoteza maisha siku ya Jumamosi.

Wachunguzi wa haki za binadamu wamesema kuwa wengi wa wahanga ni raia na mamia zaidi ya watu wengine wamekwama katika mji wa Douma wakati majeshi ya serikali yalipovamia mji huo katika jimbo la Damascus.

Serikali ya mpito

Wakati mjumbe wa kimataifa kwa ajili ya Syria Kofi Annan hakutaja majina na kusema ni juu ya Wasyria wenyewe kuamua nani wanamtaka awemo katika serikali hiyo ya umoja wa kitaifa , ameongeza. Nitashangaa kuwa Wasyria , watachagua watu ambao wana damu mikononi mwao.

US Secretary of State Hillary Rodham Clinton waves as she arrives for a meeting of the Action Group for Syria at the European headquarters of the United Nations, UN, in Geneva, Switzerland, Saturday, June 30, 2012. The United States and Russia failed on Friday to bridge differences over a plan to ease Syrian President Bashar Assad out of power, end violence and create a new government, setting the stage for the potential collapse of a key multinational conference that was to have endorsed the proposal. (Foto:Keystone, Laurent Gillieron/AP/dapd)
Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Hillary ClintonPicha: AP

Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Hillary Clinton ameweka wazi kuwa Marekani haioni Assad kuwa atakuwa na nafasi ya uongozi katika kipindi hicho cha mpito.

Assad lazima aondoke

Assad ni lazima aondoke. Hawezi kufaulu mtihani wa ridhaa ya pamoja , amesema.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Ufaransa Laurent Fabius alikuwa na msimamo kama huo , akisema, "Ni dhahiri kuwa Assad lazima aondoke".

** FILE ** Socialist Laurent Fabius delivers a speech in this Nov. 9, 2006 file photo taken in Labege, near Toulouse, southwestern France, during the final debate, before Socialist party members, among the three Socialists hoping to become France's next president. Three rivals vying to lead the Socialist Party into next year's French presidential election were wrapping up campaigning ahead of their party's primary on Thursday, with Segolene Royal favored to win the nomination. (AP Photo/Remy Gabalda, file)
Waziri wa mambo ya kigeni wa Ufaransa Laurent FabiusPicha: AP

Hakuna mtu anayeweza kudhania kwa dakika moja kuwa Assad atakuwamo katika serikali mpya, kama vile mtu anavyoweza kufikiria kuwa kuna uwezekano wa yeye kuunda mazingira yatakayokuwa hayaelemei upande wowote, kama inavyotakiwa na makubaliano hayo, amesema waziri huyo na kuongeza kuwa serikali ya mpito , itawaengua wauwaji.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Uingereza William Hague amekiri kuwa makubaliano hayo ni makubaliano ya muafaka, wakati Urusi ilichukua msimamo kuwa imeyashawishi mataifa mengine makubwa duniani kuwa haitakubalika kuyatenga makundi yoyote katika hatua hiyo ya mpito.

ITAR-TASS: MOSCOW, RUSSIA. APRIL 10, 2012. Russia_s Foreign Minister Sergei Lavrov pictured during a joint press conference with his Syrian counterpart Walid Muallem. (Photo ITAR-TASS / Sergei Fadeichev), (c) picture alliance / dpa
Waziri wa mambo ya kigeni wa Urusi Sergei LavrovPicha: picture-alliance/dpa

Urusi yamkingia kifua Assad

Urusi ikiwa ni mshirika wa muda mrefu wa Syria , inajisikia vibaya kumuweka kando Assad, hata kama mahusiano kati ya Urusi na Syria yameanza kupooza.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Urusi Sergei Lavrov amesema ," Ni vipi hasa kazi ya mpito itafanyika kuelekea katika hatua mpya itaamuliwa na Wasyria wenyewe".

Mwandishi : Sekione Kitojo /afpe

Mhariri : Sudi Mnette