1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiBurundi

Rais Ndayishimiye ataka LGBTQ kupigwa mawe

31 Desemba 2023

Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye amewataka wananchi kuwapiga mawe watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja.

https://p.dw.com/p/4ajrl
Mosambik I Diskrimierung und Gewalt gegen LGBTQ
Picha: Sitói Lutxeque/DW

Matamshi hayo yaashiria hatua kali zaidi dhidi ya jamii hiyo ya wachache nchini humo ambao tayari wanakabiliwa na ubaguzi wa kijamii na vifungo vya hadi miaka miwili jela ikiwa watapatikana na hatia ya kujihusiaha na mapenzi ya jinsia moja.

“Nafikiri hata hawa watu tukiwapata Burundi, ni bora kuwapeleka kwenye uwanja na kuwapiga mawe. Na hiyo haiwezi kuwa dhambi," alisema, akiuelezea ushoga kama unaoingizwa kutoka Magharibi.

Matamshi haya ya Ndayishimiye ni karibuni yanayoonyesha kwamba taifa hilo na mengine ya ukanda huo hayataivumilia jamii ya LGBTQ.

Uganda ilipitisha sheria kali mwezi Mei inayotoa hukumu ya kifo kwa aina fulani za makosa ya mapenzi ya jinsia moja na kifungo cha muda mrefu, hatua iliyolaaniwa vikali na serikali za Magharibi na wanaharakati wa haki za binadamu.